Featured Kitaifa

MNDEME ATAKA WANAWAKE KUTEMBEA KIFUA MBELE CCM IPO IMARA

Written by mzalendoeditor

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Tanzania Bara, Christine Mndeme,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT),Mkoa wa Dodoma uliofanyika leo Novemba 17,2022 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa UWT Dkt.Philis Nyimbi ,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT),Mkoa wa Dodoma uliofanyika leo Novemba 17,2022 jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemery Senyamule,akizungumza wakati wa  Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT),Mkoa wa Dodoma uliofanyika leo Novemba 17,2022 jijini Dodoma.

KATIBU wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT),Mkoa wa Dodoma uliofanyika leo Novemba 17,2022 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma anayemaliza muda wake, Neema Majule,akizungumza wakati wa  Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT),Mkoa wa Dodoma. uliofanyika leo Novemba 17,2022 jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Uchaguzi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri akitoa maelekezo kwa wagombea wa nafasi mbalimbali wakati wa  Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT),Mkoa wa Dodoma. uliofanyika leo Novemba 17,2022 jijini Dodoma.

…………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Tanzania Bara, Christine,amewataka Wanawake wote nchini kutembea Kifua mbele kwani Chama cha Mapinduzi CCM kipo imara.

Hayo ameyasema leo Novemba 17,2022 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT),Mkoa wa Dodoma.

Bi.Mndeme amewataka wagommbea wa nafasi mbalimbali kuzingatia mambo matano ikiwa ni pamoja na kwenda kusimamia uhai wa chama.
”Nawaomba Wanawake ppopote mlipo mtembee kifua mbele Chama kipo imara tena zaidi ya sana hivyo tuendelee kusimamia ilani ya chama chetu”amesema
Ametaja mambo mengine ya kuzingatia nia pamoja na kuzingatia  ratiba ya vikao vya kikanuni,kusimamia suala la kuongeza wanachama wapya,kujisajili kwa mfumo wa kieletroniki  na kusimamia ulipaji wa ada.
Aidha amewataka wagombea watakaochaguliwa  kwenda kusimamia iIani ya CCM pamoja na  kunena mazuri ya ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UWT Dkt.Philis Nyimbi  amewaasa wanawake kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuwaletea watanzania maendeleo.
Awali,Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma anayemaliza muda wake, Neema Majule amesema kama Jumuiya katika kipindi cha miaka mitano wameweza kufanya siasa na uchumi kwa kuanzisha shule ya chekechekea na kujenga fremu za maduka.
Mkutano huo unawashirikisha wajumbe 536 ambapo jumla ya wanachama wanne wamepitishwa kugombea nafasi hiyo ambao ni Neema Majule, Kaundime Kasase, Elizabeth Lameck na Zabibu Mafta.

About the author

mzalendoeditor