Featured Kitaifa

MBUNGE MTATURU AIBANA SERIKALI

Written by mzalendoeditor

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameihoji serikali ni lini itapeleka kiasi cha fedha kilichotengwa Shilingi Bilioni 1.1 kwa ajili ya kujenga kituo cha polisi cha Ikungi ili ujenzi huo uanze mara moja.

“Mh spika tulipitisha hapa bungeni bajeti ya Shilingi Bilioni 1.1 kwa ajili ya kujenga kituo cha polisi pale Ikungi,ninavyozungumza leo ni mwezi wa 11,je ni lini serikali italeta fedha kwa ajili ya kujenga kituo hicho,?amehoji.

Akijibu swali hilo Novemba 10,2022,Bungeni Jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini amekiri kuwa ni kweli bajeti hiyo ilipitishwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.

“Kinachofanyika ni kwamba Jeshi la Polisi limewasilisha mpango kazi wa ujenzi ambao utakapopitishwa na wizara utawasilishwa hazina kwa ajili ya kuidhinisha fedha,

“Ni imani yetu fedha za maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiki kwa vile zinatoka kwenye mfuko ambao tuliuzungumzia kikamilifu wiki iliyopita, zitatoka kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa kituo hicho kuanza ,”amesema Sagini.

About the author

mzalendoeditor