Featured Kitaifa

MAJALIWA AKAGUA KAZI YA KUFUFU NA KUSAFISHA VISIMA VYA MAJI SAFI JIJINI DAR ES SALAAM

Written by mzalendoeditor

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya  Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Cyprian Luhemeja  (kushoto)  wakati alipokagua  visima vya dharura  vinavyosafishwa na kufufuliwa  na kuunganishwa kwenye mfumo wa huduma ya maji kwa wananchi katika eneo la Mwananyamala Komakoma jijini Dar es salaam , Novemba 10, 2022. Wa nne kulia ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange   na wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Dar es salaam, Kate Kamba.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia maji yaliyokuwa yakibubujika  wakati  alipokagua  visima vya dharura  vinavyosafishwa, kufufuliwa na  kuunganishwa kwenye mfumo wa huduma maji kwa wananchi katika eneo la Tabata Relini  jijini Dar es salaam , Novemba 10, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

About the author

mzalendoeditor