MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Dkt.Anselm Moshi,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Bodi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 24,2022 jijini Dodoma.
………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Dkt.Anselm Moshi amesema kuwa wana mpango wa kuanza kutumia teknolojia ya kuzalisha mafuta ya kupikia yatokanayo na Pumba za Mpunga kupitia kiwanda chake cha Mkuyuni jijini Mwanza.
Hayo amesemwa leo Oktoba 24,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za bodi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Dkt. Moshi amesema kuwa kwasasa wapo katika upembuzi yakinifu katika kuongeza thamani mazao ya mpunga ili kuweza kuzalisha mafuta yatokanayo na Pumba za Mpunga.
“Tuna mpango wa kuanza kutumia teknolojia ya kuzalisha mafuta ya kupikia yatokanayo na pumba za mpunga kupitia kiwanda chetu kilichopo Mkuyuni jijini Mwanza,”amesema Dkt.Moshi
Pia amesema kuwa wana mpango wa kuzalisha kuni kupitia pumba za Mpunga katika kupunguza uharibifu wa mazingira.
Aidha,amesema kuwa kwa Mwaka 2021/2022 wamenunua mazao Tan Elfu 26,665,000 yenye Thamani ya shillingi Billion 14.8 na kuongeza Thamani mazao Tan 16,000.3 yenye Thamani Billion 8.2.
Dkt.Moshi amesema kuwa CPB imedhamiria kuwafikia wakulima wengi zaidi ili wazalishe kwa ufanisi shambani.
“Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko PCB dhamira yake ni kuwawezesha wakulima kulima kwa kutumia mbinu za kisasa kwa maslahi yao binafsi na Taifa kwa ujumla,”amesema
Dkt. Moshi amesema kuwa ili mkulima apate mapato mengi anatakiwa kulima kwa Tija na kuendana na soko la kibiashara.
Hata hivyo ameeleza kuwa kwasasa wanatekeleza Kilimo cha mikataba kwa baadhi ya mazao hususani zao la ngano ili kupungza uagizaji wa ngano kutoka nje ya nchi ambapo kwasasa serikali inaagiza zao hilo kwa kiwango kikubwa kutoka nje ya nchi.
”Kwa sasa bodi inatekeleza Kilimo cha mkataba wa mazao mbalimbali ikiwemo zao la ngano ili kupunguza uagizaji wa zao hilo kutoka nje ya nchi.”amesema Dkt.Moshi
Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), ni Taasisi ya serikali chini ya wizara ya Kilimo iliyopewa dhamana ya kufanya biashara ya nafaka na mazao mchanganyiko na imeanzishwa kwa sheria ya nafaka na mazao changanyiko Namba 19 ambapo pia hadi sasa mzunguko wa biashara katika taasisi hiyo umeongezeka kutoka bilioni 15 hadi bilioni 52,”amesema Dkt.Moshi.
MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Dkt.Anselm Moshi,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Bodi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 24,2022 jijini Dodoma.
MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Dkt.Anselm Moshi,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kutoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 24,2022 jijini Dodoma.