Featured Kitaifa

MRADI UJENZI WA UWANJA MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA NA KITUO CHA MIKUTANO NA HOTELI KUIMARISHA UCHUMI WA ZANZIBAR

Written by mzalendoeditor

KATIBU Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Amour Hamil Bakar (kushoto) akitiliana saini hati za makubaliano ya kufanya upembuzi yakinifu wa miradi ya ujenzi wa kituo cha mikutano na maonesho ya biashara kimataifa na Mkurugenzi Mtendaji Afrika Mashariki wa kampuni ya Elsewedy Electric, Mhandisi Ibrahim Qamarkatika ofisi za wizara hiyo Kinazini.

………………………

NA MWANDISHI WETU
WIZARA ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda imeeleza kuwa kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa uwanja wa maonesho ya biashara ya kimataifa na kituo cha mkutano na hoteli, kutaimarisha uchumi wa Zanzibar.
Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini wa makubaliano ya utekelezaji wa upembuzi katika ofisi za wizara hiyo Kinazini, Waziri wa hizara hiyo, Omar Said Shaaban, alieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuirudisha Zanzibar katika hadhi yake kibiashara.
Alieleza kuwa kusainiwa kwa makubaliano hayo kunakwenda kutekeleza ndoto za Zanzibar kuwa na kumbi za mikutano za kimataifa zinazoweza kuchukua idadi kubwa ya watu na vifaa vya kisasa kutekeleza dhana ya uchumi wa buluu.
Alieleza kuwa ukumbi huo pamoja na hoteli ya kisasa vitajengwa Mbweni wakati kituo cha maonesho ya biashara kitakachojengwa Nyamanzi, wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja, kinalenga kusisimua biashara na kuirudisha Zanzibar kuwa kitovu cha biashara.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya Elsewedy, Mhandisi Qamar alieleza kufurahishwa na hatua hiyo ambayo ni matokeo utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano yaliyofanywa na kampuni mbali mbali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, mjini Dubai.
“Wakati wa maonesho ya Dubai mapema mwaka huu, kampuni kadhaa zilitia saini makubaliano na Rais Samia Suluhu Hassan kwa miradi kadhaa, sisi (Elsewedy Electric) tuliamua kuja Zanzibar kuanza uwekezaji kwenye maeneo haya mawili, kama tulivyofanya Tanzania bara,” alieleza Mhandisi Qamar.
Alifafanua kwamba makubaliano hayo yanahusu upembuzi yakinifu, usanifu, uhandisi, ununuzi na kazi za ujenzi kwa miradi yote miwili kazi ambayo itafadhiwa kampuni hiyo na kutekelezwa katika kipindi cha miezi sita kuanzia sasa.
“Tunaamini kazi hii itakamilika ndani ya muda ili tuanze kazi kubwa zaidi ambayo tunaamini kwa mashirikiano tunayoyapata kutoka wizarani tutafanikisha ndoto za serikali na kampuni yetu ambayo imewekeza sehemu mbali mbali afrika,” alileza Mhandisi Qamar.
Alieleza kuwa wamejipanga kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa wakati kabla ya kukubaliana namna ya kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo inayokadiriwa kutumia zaidi ya dola milioni 100 za marekani.

KATIBU Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Amour Hamil Bakar (kushoto) akitiliana saini hati za makubaliano ya kufanya upembuzi yakinifu wa miradi ya ujenzi wa kituo cha mikutano na maonesho ya biashara kimataifa na Mkurugenzi Mtendaji Afrika Mashariki wa kampuni ya Elsewedy Electric, Mhandisi Ibrahim Qamarkatika ofisi za wizara hiyo Kinazini.

KATIBU Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Amour Hamil Bakar (kushoto) akibadilishana hati za makubaliano ya kufanya upembuzi yakinifu wa miradi ya ujenzi wa kituo cha mikutano na maonesho ya biashara kimataifa na Mkurugenzi Mtendaji Afrika Mashariki wa kampuni ya Elsewedy Electric, Mhandisi Ibrahim Qamar katika ofisi za wizara hiyo Kinazini.

Mkurugenzi Mtendaji Afrika Mashariki wa kampuni ya Elsewedy Electric, Mhandisi Ibrahim Qamar, akizungumza baada ya kutiliana saini hati za makubaliano ya kufanya upembuzi yakinifu wa miradi ya ujenzi wa kituo cha mikutano na maonesho ya biashara kimataifa na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar. Kushoto ni Waziri wa wizara hiyo Omar Said Shaaban.

WAZIRI wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban (kushoto) akizungumza na ujumbe kutoka kampuni ya Esewedy Electric ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Mhandisi Ibrahim Qamar, mara baada ya kutiliana saini hati za makubaliano ya kufanya upembuzi yakinifu wa miradi ya ujenzi wa kituo cha mikutano na maonesho ya biashara kimataifa na kampuni hiyo uliofanyika katika ofisi za wizara hiyo Kinazini.

WAZIRI wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban (kushoto) akisalimiana na ujumbe kutoka kampuni ya Esewedy Electric ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Mhandisi Ibrahim Qamar, mara baada ya kutiliana saini hati za makubaliano ya kufanya upembuzi yakinifu wa miradi ya ujenzi wa kituo cha mikutano na maonesho ya biashara kimataifa na kampuni hiyo uliofanyika katika ofisi za wizara hiyo Kinazini.

About the author

mzalendoeditor