Featured Michezo

SERENGETI GIRLS YAICHAPA UFARANSA KOMBE LA DUNIA

Written by mzalendoeditor
TANZANIA imeonyesha uimara katika michuano ya Kombe la Dunia Wasichana U17 baada ya kuwachapa Ufaransa mabao 2-1 leo katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Jawaharlal Nehru, Margao, Goa nchini India.
Mabao ya Serengeti Girls yamefungwa na Diana Mnally dakika ya 16 na Christer Bahera dakika ya 56 kwa penalti,.
 Ufaransa  walipata bao la kufutia machozi dakika ya 75 likifungwa na Lucie Calba  ,Serengeti girls watacheza na Canada Siku ya Jumanne huku wakihitaji ushindi au sare ili waweze kutinga robo fainali ya Michuano hiyo.

Ikumbukwe Serengeti Girls ilianza vibaya michuano hiyo kwa kuchapwa 4-0 na Mabingwa watetezi, Japan. 

About the author

mzalendoeditor