Featured Michezo

BONANZA LA MAPINDUZI SPORTS CLUB LAFANA JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

Katibu wa NEC Organaizesheni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Dk Maudline Castico,akiongoza  bonanza la kuadhimisha  miaka 23 ya kifo cha  Mwalimu Nyerere lilofanyika katika viwanja vya Mtekelezo na Jamhuri  leo Oktoba 14,2022 Jijini Dodoma.

………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

KATIBU wa NEC Organaizesheni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Dk Maudline Castico,ameongoza bonanza la kuadhimisha miaka 23 ya kifo cha  Mwalimu Nyerere huku akisema wamejipanga kuendeleza michezo mbalimbali aliyokuwa akiipenda.

Akizungumza leo Oktoba 14 2022 jijini Dodoma wakati wa bonanza hilo lilofanyika katika viwanja vya Mtekelezo na Jamhuri,ambapo amesema kuwa suala la michezo ni muhimu kwani linawaunganisha watu wote.

”CCM itaendelea kuenzi mambo mazuri  yaliyofanywa na hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo kuendeleza michezo aliyokuwa akiipenda kama bao na netiboli.”amesema Dk.Castico

Bonanza hilo limeshirikisha michezo mbalimbali kama vile Mchezo wa Mpira wa Miguu,Netiboli,kuvuta kamba,riadha kwa wazee na vijana,drafti na bao na washiriki walikuwa wafanyakazi wa CCM na wanamichezo mbalimbali.

Dk Castico ameeleza kuwa  Mwalimu Nyerere alikuwa akipenda michezo hivyo ni lazima wamuenzi kwa vitendo ikiwemo kufanya mazoezi.

Amesema kutokana na umuhimu wa michezo ni lazima kuwe na Programu maalum za kuhakikisha watu wanafanya mazoezi.

“Programu za michezo zijulikane kwa makundi yote.Rais (Samia Suluhu Hassan)  anathamini michezo ndio maana kuna watu wapo Olimpiki.Mimi nimefurahi sana kwa jinsi ambavyo mmeandaa bonanza hili katika hili tunawaunga mkono,”amesema Katibu huyo.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa  Mapinduzi Sc,Kajoro Vyohoroka,amesema kuwa lengo la bonanza hilo ni kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na Mwalimu Nyerere ikiwemo unzishwaji wa timu ya Mapinduzi.

”Timu hiyo iliasisiwa miaka 47 iliyopita na Mwalimu Nyerere,Rashidi Kawawa na Moses Nnauye  na ilikuwa ikifanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya netiboli.”amesema Vyohoroka

Naye Katibu Msaidizi wa NEC Organaizesheni Zakaria Mwansasu amesema wamejipanga kuifufua timu hiyo.

Mwansasu amesema kuwa Mapinduzi ilikuwa ikishiriki ligi draja la kwanza na mashindano mbalimbali  na miaka ya nyuma ilisifika  kwa kuwa na wachezaji wenye vipaji.

“Wale waliokuwa wachezaji wetu miaka hiyo kwa sasa wamezeeka tunatafuta vipaji vipya ili turudishe heshima yetu kama ilivyokuwa miaka ya zamani,”amesema Bw.Mwansasu

Awali Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma,Pili Mbaga,amewapongeza waandaaji wa bonanza hilo  pamoja na wanamichezo mbalimbali walioshiriki.

”Tunawapongeza waandaaji wa bonanza hilo ambalo limetukutanisha wadau mbalimbali katika kumuezi Baba wa Taifa ambaye alikuwa anapenda michezo hivyo CCM lazima tuendelee kuyaenzi yale mazuri aliyokuwa akiyafanya”amesema

Katibu wa NEC Organaizesheni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Dk Maudline Castico,akiongoza  bonanza la kuadhimisha  miaka 23 ya kifo cha  Mwalimu Nyerere lilofanyika katika viwanja vya Mtekelezo na Jamhuri  leo Oktoba 14,2022 Jijini Dodoma.

Katibu wa NEC Organaizesheni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Dk Maudline Castico,(hayupo pichani) akishuhudia mchezo wa kukimbia na magunia wakati wa bonanza la kuadhimisha  miaka 23 ya kifo cha  Mwalimu Nyerere lilofanyika leo Oktoba 14,2022 Jijini Dodoma katika viwanja vya Mtekelezo na Jamhuri

Katibu wa NEC Organaizesheni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Dk Maudline Castico,(hayupo pichani) akishuhudia mchezo wa kukimbiza kuku wakati wa bonanza la kuadhimisha  miaka 23 ya kifo cha  Mwalimu Nyerere lilofanyika leo Oktoba 14,2022 Jijini Dodoma katika viwanja vya Mtekelezo na Jamhuri

Katibu wa NEC Organaizesheni Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk Maudline Castico,(akimchambua golikipa kwa Penalti kuashiria kuanza kwa mchezo wa Mpira wa Miguu kati ya Mapinduzi Sports Club dhidi ya Chang’ombe ambapo Chang’ombe wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 wakati wa bonanza la kuadhimisha  miaka 23 ya kifo cha  Mwalimu Nyerere lilofanyika leo Oktoba 14,2022 Jijini Dodoma katika viwanja vya Mtekelezo na Jamhuri.

Katibu wa NEC Organaizesheni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Dk Maudline Castico,akisalimiana na timu ya  Mapinduzi Sports  Club na  Chang’ombe kabla ya kuanza kwa mtanange huo ambapo Chang’ombe wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 wakati wa bonanza la kuadhimisha  miaka 23 ya kifo cha  Mwalimu Nyerere lilofanyika leo Oktoba 14,2022 Jijini Dodoma katika viwanja vya Mtekelezo na Jamhuri.

Kikosi cha Mapinduzi Sports Club kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuwavaa wapinzani wake timu ya Chang’ombe.

Kikosi cha Timu ya Chang’ombe kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuwaa Mapinduzi Sport Club.

Katibu wa NEC Organaizesheni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Dk Maudline Castico,(hayupo pichani) akishuhudia mchezo wa Mpira wa Miguu kati ya Mapinduzi Sports Club dhidi ya Chang’ombe ambapo Chang’ombe wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 wakati wa bonanza la kuadhimisha  miaka 23 ya kifo cha  Mwalimu Nyerere lilofanyika leo Oktoba 14,2022 Jijini Dodoma katika viwanja vya Mtekelezo na Jamhuri.

Katibu wa NEC Organaizesheni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Dk Maudline Castico,(hayupo pichani) akishuhudia mchezo wa  Netboli kati ya Mapinduzi Queens dhidi ya  jiji la Dodoma ambapo Mapinduzi Queens wameibuka na ushindi wa vikapu 25-17 wakati wa bonanza la kuadhimisha  miaka 23 ya kifo cha  Mwalimu Nyerere lilofanyika leo Oktoba 14,2022 Jijini Dodoma katika viwanja vya Mtekelezo na Jamhuri.

Katibu wa NEC Organaizesheni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Dk Maudline Castico,(hayupo pichani) akishuhudia Mchezo ya Kuvuta kamba pamoja na Mchezo wa bao wakati wa bonanza la kuadhimisha  miaka 23 ya kifo cha  Mwalimu Nyerere lilofanyika leo Oktoba 14,2022 Jijini Dodoma katika viwanja vya Mtekelezo na Jamhuri.

Katibu wa NEC Organaizesheni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Dk Maudline Castico,akizungumza mara baada ya kumalizaka kwa michezo mbalimbali wakati wa bonanza la kuadhimisha  miaka 23 ya kifo cha  Mwalimu Nyerere lilofanyika leo Oktoba 14,2022 Jijini Dodoma katika viwanja vya Mtekelezo na Jamhuri.

Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma,Pili Mbaga,akizungumza wakati wa bonanza la kuadhimisha  miaka 23 ya kifo cha  Mwalimu Nyerere lilofanyika leo Oktoba 14,2022 Jijini Dodoma katika viwanja vya Mtekelezo na Jamhuri.

Katibu Msaidizi Mkuu,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zakaria Mwansasu,akizungumza wakati wa bonanza la kuadhimisha  miaka 23 ya kifo cha  Mwalimu Nyerere lilofanyika leo Oktoba 14,2022 Jijini Dodoma katika viwanja vya Mtekelezo na Jamhuri.

Mwenyekiti wa  Mapinduzi Sports Club,Kajoro Vyohoroka,akizungumza wakati wa bonanza la kuadhimisha  miaka 23 ya kifo cha  Mwalimu Nyerere lilofanyika leo Oktoba 14,2022 Jijini Dodoma katika viwanja vya Mtekelezo na Jamhuri.

Katibu wa NEC Organaizesheni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Dk Maudline Castico,akitoa zawadi mbalimbali kwa washindi mara baada ya kumalizaka kwa  bonanza la kuadhimisha  miaka 23 ya kifo cha  Mwalimu Nyerere lilofanyika leo Oktoba 14,2022 Jijini Dodoma katika viwanja vya Mtekelezo na Jamhuri.

About the author

mzalendoeditor