Featured Kitaifa

OWMS YAPUNGUZA MIGOGORO DHIDI YA SERIKALI ILIYOFUNGULIWA KWENYE MAHAKAMA NA MABARAZA YA NJE NA NDANI YA NCHI

Written by mzalendoeditor

NAIBU Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende,akizungumza  wakati akizindua Baraza la kwanza la wafanyakazi wa OWMS kwa mwaka wa fedha 2022/23 lililofanyika leo Oktoba 13,2022 jijini Dodoma.

……………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

NAIBU Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende,ameeleza kuwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS) imepunguza idadi ya migogoro dhidi ya Serikali iliyofunguliwa kwenye Mahakama na mabaraza ya nje na ndani ya nchi.

Hayo ameyasema leo Oktoba 13,2022 jijini Dodoma wakati akizindua Baraza la kwanza la wafanyakazi wa OWMS kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Dkt.Luhende amesema kwa kipindi cha miaka minne ofisi hiyo imekuwa ikiwakilisha serikali mahakamani na katika mabaraza ya usuluhishi ambapo imeendesha mashauri 6,043 ambapo ya madai 5885 na ya usuluhishi 158.

“Mashauri ya Madai yaliyomalizika katika kipindi cha miaka minne upande wa madai ni 582 na ya usuluhishi ni 60. Kati ya hayo, Serikali imeshinda mashauri 530 ya madai na Mashauri ya Usuluhishi 31,”amesema

Amesema kuwa kama alivyoagiza na Rais  Samia Suluhu Hassan, OWMS imeendelea kuhakikisha inaiwakilisha vyema Serikali na kuvutia wawekezaji nchini kwa kumaliza migogoro mbalimbali dhidi ya wawekezaji na wafanyabiashara kwa njia ya majadiliano

” Jambo ambalo limesaidia kupunguza idadi ya migogoro dhidi ya Serikali iliyofunguliwa kwenye Mahakama na mabaraza nje na ndani,kuokoa fedha za Serikali ambazo zingetumika katika kuendesha migogoro tajwa, kudumisha uhusiano kati ya Serikali na wawekezaji”amesema.

Pia amesma kujenga imani kwa wawekezaji kuhusu hali ya utoaji haki nchini, pamoja na kukuza diplomasia ya uchumi.

“Mfano wa shauri la usuluhishi lililomalizika kwa njia ya majadiliano ni baina ya G.S Engineering &Construction Corporation ya Korea ya Kusini dhidi ya TANROADS likihusiana na ujenzi wa daraja la Tanzanite na mgogoro ulikuwa umepelekwa ICC na shauri lilimalizika na sasa daraja linaendelea kutoa huduma kwa wananchi,” amesema Dkt. Luhende.

Kwa upande wake Naye Wakili wa Serikali Mwandamizi, Bi Jenipher Kaaya amesema kuwa OWMS imefanikiwa kumaliza mashauri nje ya mahakama au mabaraza ya usuluhishi kwa kufanya majadiliano na wale wanaoidai Serikali kwa kuweka masuala ya kisheria pembeni na kujadili hoja kama watu wa kawaida na hatimaye kufika mwafaka na kuweza kushinda mashauri hayo.

Naye, Mmoja wa wajumbe wa baraza hilo, Rashid Mohamed kutoka Tanga, amesema baraza hilo ni muhimu katika kuimarisha utendaji kazi.

NAIBU Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende,akizungumza  wakati akizindua Baraza la kwanza la wafanyakazi wa OWMS kwa mwaka wa fedha 2022/23 lililofanyika leo Oktoba 13,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa OWMS, James Kibamba,akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Baraza la kwanza la wafanyakazi wa OWMS kwa mwaka wa fedha 2022/23 lililofanyika leo Oktoba 13,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende (hayupo pichani) wakati akizindua Baraza la kwanza la wafanyakazi wa OWMS kwa mwaka wa fedha 2022/23 lililofanyika leo Oktoba 13,2022 jijini Dodoma.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Bi Jenipher Kaaya,akielezea jinsi walivyofanikiwa kumaliza migogoro mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Baraza la kwanza la wafanyakazi wa OWMS kwa mwaka wa fedha 2022/23 lililofanyika leo Oktoba 13,2022 jijini Dodoma.

Mmoja wa Wajumbe wa Baraza hilo, Wakili wa Serikali, Rashid Mohamed,akizungumzia mafanikio yaliyopatikana kutoka OWMS wakati wa uzinduzi wa Baraza la kwanza la wafanyakazi wa OWMS kwa mwaka wa fedha 2022/23 lililofanyika leo Oktoba 13,2022 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor