Featured Kitaifa

SERIKALI YAJA NA MIKAKATI KUFUFUA VITUO VYA WALIMU NCHI NZIMA

Written by mzalendoeditor

Serikali imesema imeweka mkakati wa kufufua vituo vya walimu (Teachers Resource Centers) vya nchi nzima ili kuwawezesha walimu kupata sehemu ya kukutana na kubadilishana uzoefu pamoja na kujiendeleza kwa kujisomea

Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda wilayani Bukombe wakati akiongea na walimu wa wilaya hiyo katika kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani ambapo amesema mbali ya kufufua vituo hivyo pia inaendelea kutoa mafunzo kazini kwa walimu.

Prof. Mkenda amesema walimu wameandaliwa vizuri vyuoni lakini hiyo haitoshi kwa kuwa kila siku mambo yanabadilika na walimu wanapaswa kuendelea kujifunza kila mara ili kuwa na mbinu sahihi za ufundishaji kulingana na wakati.

“Walimu wetu ni wazuri sana na wanaandaliwa vyema vyuoni lakini haitoshi tunapaswa kuhakikisha wanapata mafunzo kazini ya mara kwa mara na wizara ya elimu imetenga fedha kwa ajili ya kutoa mafunzo kazini kwa walimu,: amesema Pro. Mkenda.

Amewataka walimu pia kutumia vituo vya Chuo Kikuu Huria kujiendeleza pamoja na kuchangamkia fursa za masomo zaidi ya elimu ya juu kufuatia ujenzi wa kampasi mpya 14 za vyuo vikuu mbalimbali zitakazojengwa na Wizara kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) katika Mikoa 14

Aidha, amewaeleza walimu hao kuwa Serikali ipo katika kufanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 pamoja na
mabadiliko ya mitaala yanayolenga katika kuhakikisha elimu bora na yenye kuzingatia Ujuzi inatolewa.

Amewataka walimu hao kujiandaa kutekeleza mitaala itakayokuwa imefanyiwa mabadiliko kwani wao ndio nguzo kuu na kuwa Setikali imejipanga kuwandaa walimu wote nchini kutekeleza mtaala huo pindi utakapo kamilika.

Naye Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amemwambia Waziri wa Elimu kuwa wilaya hiyo ina walimu ambao wanajituma na kufanya kazi kwa bidii bila kujali changamoto wanazokutana nazo.

Pia Waziri Biteko amemwomba Prof. Mkenda kuipatia wilaya hiyo chuo cha VETA kwa kuwa ina shule za Sekondari ambazo kila mwaka zinazalisha wahitimu wa kidato cha nne na sita ambao wengine wanaweza kujiunga na mafunzo ya ufundi.

Mkuu wa mkoa wa Geita Martin Shigela ameishukuru Wizara ya elimu kwa kuzipatia kuupatia Mkoa wa Geita fedha Chui cha VETA cha Wilaya ya Chato na VETA ya Mkoa inaendelea inayoendelea kujengwa Wilayani Geita.

About the author

mzalendoeditor