Featured Kitaifa

SIKU 558 ZA SAMIA MADARAKANI MISINGI YA FALSAFA ZA UCHUMI KUONGOZA UCHUMI ZAFANIKIWA- MWENEZI SHAKA

Written by mzalendoeditor


KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema ndani ya siku 558 tangu Rais Samia Suluhu Hassan aapishwe kuwa Rais wa Tanzania, amefanikiwa kutekeleza falsafa ya uchumi kuongozwa kwa misingi ya kiuchumi..

Shaka ameyasema hayo leo Oktoba 9, 2022, Kibaha mkoani Pwani alipotembelea Maonesho ya Tatu ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani amesema misingi hiyo ni pamoja na kuvutia wawekezaji, ushirikishaji sekta binafsi na kutumia diplomasia badala ya mabavu katika kufungua uchumi.

“Leo ni takribani siku 558 tangu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aapishwe kuwa Rais wa nchi yetu, ambapo baada ya kiapo alitoa mwelekeo wa serikali atakayoiunda na kuiongoza kuwa, nia yake ni kuifungua nchi kiuchumi.

“Sote ni mashuhuda tumeanza kushuhudia akiruhusu misingi ya falsafa za uchumi kuongoza uchumi badala ya nguvu za kiutawala. Tumeshuhudia Rais Samia akitumia taaluma yake ya uchumi na uzoefu wake wa kiuongozi na masuala ya kidiplomasia akibadili kabisa mazingira na kasi ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo,” amesema.

Shaka amesema ndani ya kipindi hicho kupitia diplomasia ya uchumi Rais Samia amefanikiwa kutafuta na kuvutia wawekezaji, kuimarisha mazingira ya biashara na kuongeza shughuli za uzalishaji zitakazoongeza ajira na mapato ya serikali.

Aidha, amesema ameimarisha mazingira ya bishara na uwekezaji kwa kuondoa urasimu, ukusanyaji kodi wa mabavu, kufanya maboresho ya sheria na mifumo mbalimbali kwa lengo la kuondoa kero kwa wafanyabiashara na wawekezaji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ibara 22, 46 na 49.

Akiwa katika maonyesho hayo, Shaka ambaye aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri ametembelea mabanda mbalimbali yanayoshiriki maonesho hayo yakiwamo ya taasisi za umma, binafsi na wajasiriamali.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akiwapungia mkono baadhi ya Washiriki wa maonesho ya tatu ya Uwekezaji na Biashara (hawapo pichani) alipokuwa akiendelea kukagua baadhi ya Mabanda ya Maonesho hayo alipotembelea leo Oktoba 9, 2022, Kibaha mkoani Pwani .Pichani nyuma ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas Ahmed na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Sarah Msafiri . PICHA ZOTE NA MICHUZI JR

Afisa Mipango Mwandamizi Idara ya Miundombinu na Uwezeshaji – Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) akieleza shughuli mbalimbali na mipango ya maendeleo kuhusu Mamlaka hiyo kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka (wa pili kulia),wakati akipita na kukagua baadhi ya Mabanda ya Maonesho alipotembelea Maonesho ya Tatu ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani leo Oktoba 9, 2022, Kibaha mkoani Pwani.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Sarah Msafiri

Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe.Sarah Msafiri akifafanua jambo kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka alipotembelea banda la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),katika Maonesho ya Tatu ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani leo Oktoba 9, 2022, Kibaha mkoani Pwani
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akipata maelezo kuhusu mbegu za miwa kutoka kwa Mratifu wa Utafiti wa Miwa kitaifa kutoka Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI),Minza Masunga,alipotembelea banda la Taasisi hiyo leo kwenye maonesho ya Tatu ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akimsikiliza Meneja Utawala wa Taasisi ya Aba Alliance, Elizabeth Buberwa kuhusu shughuli mbalimbali wazifanyazo alipotembelea banda hilo leo kwenye maonesho ya Tatu ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani,kulia ni Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Sarah Msafiri.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akimsikiliza Mwenyekiti wa Kampuni ya Ujenzi ya Group Six International Ltd Janson Huang kuhusu namna walivyojipanga katika masuala ya uwekezaji nchini, alipotembelea banda hilo leo kwenye maonesho ya Tatu ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR



About the author

mzalendoeditor