Featured Michezo

TAMISEMI HAISHIKIKI SHIMIWI,YAIZAMISHA RAS SHINYANGA

Written by mzalendoeditor

Timu ya wanawake ya kuvuta kamba ya TAMISEMI imeshinda 2-0 dhidi ya mpinzani wake timu ya Ras Shinyanga katika michezo inayoendelea ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Jijini Tanga.

Mechi hiyo iliyochezwa leo Oktoba 6, 2022 katika viwanja vya shule ya Sekondari Usagara.

Timu ya TAMISEMI wanawake ya kuvuta kamba inaendelea kufanya vizuri katika mechi na mpaka sasa wanaongoza kufanya vizuri kwa hatua ya makundi.

TAMISEMI imeshacheza mechi na MSD, Wizara ya Mambo ya Nje na RAS –Shinyanga na mechi zote hizo walizocheza wamekuwa ni washindi.

About the author

mzalendoeditor