Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Mawakili wa Serikali kabla ya kuzindua Chama cha Mawakili wa Serikali, nembo na Mfumo rasmi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hafla iliyofanyika leo Septemba 29,2022 Jijini Dodoma.
…………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaagiza mawakili wa serikali nchini kusisimamia haki kwa kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyatatua kwa kufuata misingi na miongozo ya sheria na kumaliza baadhi ya kesi bila kuzifikisha mahakamani.
Rais Samia ametoa agizo hilo leo Septemba 29,2022 jijini Dodoma wakati akizindua chama cha mawakili wa serikali,nembo ya ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na mfumo rasmi wa ofisi hiyo katika mkutano mkuu wa mawakili wa serikali ambapo amewasisitiza mawakili wa serikali kutenda haki kwa kufuata miongozo ya sheria.
Rais Samia amewaagiza kusimamia haki wanapochezesha vifungu vya sheria wasiwanyime wanaostahili kupata haki.
“ Ninyi ni engineer(Wahandisi) wa kucheza na vifungu vya sheria, mtu anakosa mnacheza na vifungu anaachiwa au asiyenakosa akatiwa hatiani, sasa hiyo engineering haiwapeleki pazuri fanyeni yale yatakayowasimamisha kwenye haki.”amesema Rais Samia
Aidha Rais Samia amemuagiza AG kuweka muda maalum wa mwisho wa kujisajili Mawakili wa serikali kwenye rejista na kwa wale ambao muda utapita bila kujisajili hawatatambulika.
Kwa upande wake Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dk.Damas Ndumbaro amesema kuwa Mawakili hao ndio watekelezaji wa majukumu na askari na wapiganaji katika mfumo wa utoaji haki, masuala ya mikataba na usuluhishi wa migogoro.
Naye, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, amesema sababu za Serikali kupoteza kesi nyingi za madai ni kukosa ushirikiano wa dhati kwa baadhi ya maofisa wa Serikali hasa wakati wa kutoa ushahidi mahakamani.
”Kukosekana kwa ushirikiano wa ushahidi kwa baadhi ya maafisa wa serikali ni moja ya changamoto inayosababisha serikali kushindwa kesi mbalimbali”amesema Dk.Feleshi
Awali Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shaaban Ramadhan Abdalla, amesema wamekuwa wakishirikiana na Ofisi ya AG kushughulikia kesi na migogoro mbalimbali ya kimataifa kwa kuweka mbele uzalendo na utaifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitembelea mabanda mbalimbali likiwemo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kujionea shughuli mbalimbali pamoja na huduma zitolewazo na Ofisi hizo kabla ya kuhutubia na kuzindua Rasmi Chama cha Mawakili wa Serikali, nembo na Mfumo rasmi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Mawakili wa Serikali kabla ya kuzindua Chama cha Mawakili wa Serikali, nembo na Mfumo rasmi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hafla iliyofanyika leo Septemba 29,2022 Jijini Dodoma.
Viongozi mbalimbali pamoja na Mawakili wa Serikali wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Mawakili wa Serikali kabla ya kuzindua Chama cha Mawakili wa Serikali, nembo na Mfumo rasmi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hafla iliyofanyika leo Septemba 29,2022 Jijini Dodoma.
Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dk.Damas Ndumbaro,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mkuu Cha ma cha Mawakili wa Serikali pamoja na uzinduzi wa mfumo,Nembo na Chama cha Mawakili wa Serikali hafla iliyofanyika leo Septemba 29,2022 jijini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi,akitoa taarifa wakati wa Mkutano wa Mkuu Cha ma cha Mawakili wa Serikali pamoja na uzinduzi wa mfumo,Nembo na Chama cha Mawakili wa Serikali hafla iliyofanyika leo Septemba 29,2022 jijini Dodoma.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shaaban Ramadhan Abdalla, akizungumza wakati wa Mkutano wa Mkuu Cha ma cha Mawakili wa Serikali pamoja na uzinduzi wa mfumo,Nembo na Chama cha Mawakili wa Serikali hafla iliyofanyika leo Septemba 29,2022 jijini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Andrew Chenge,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mkuu Cha ma cha Mawakili wa Serikali pamoja na uzinduzi wa mfumo,Nembo na Chama cha Mawakili wa Serikali hafla iliyofanyika leo Septemba 29,2022 jijini Dodoma.
Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Hamis Juma,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mkuu Cha ma cha Mawakili wa Serikali pamoja na uzinduzi wa mfumo,Nembo na Chama cha Mawakili wa Serikali hafla iliyofanyika leo Septemba 29,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wakati wa Mkutano wa Mkuu Cha ma cha Mawakili wa Serikali pamoja na uzinduzi wa mfumo,Nembo na Chama cha Mawakili wa Serikali hafla iliyofanyika leo Septemba 29,2022 jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kwenye laptop kuzindua mfumo rasmi wa Kieletroniki wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (OAGMIS), nembo ya Ofisi hiyo pamoja na Chama cha Mawakili wa Serikali katika Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.