Featured Kitaifa

MRADI WA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA MIMEA NA USALAMA WA CHAKULA NCHINI WAZINDULIWA DODOMA

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde,akizindua mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

…………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI kwa kushirikiana na Shirika Umoja wa Mataifa la Chakula Duniani (FAO) na Umoja wa Ulaya (EU) imezindua mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini.

Akizungumza  leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma mara baada ya kuzindua mradi huo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde amesema mradi huo utasaidia katika kudhibiti visumbufu vigeni kwa kuhakikisha mazao yanayoingia au kutoka hapa nchini yanakuwa na ubora unaokidhi viwango vya kimataifa.

Mavunde amesema kuwa mradi huo una lengo la kuhakikisha usalama wa Chakula na kuimarisha mfumo wa ukaguzi wa utoaji wa usafi wa Mazao yanayoingia na kutoka  nchini.

“Niwashukuru EU na FAO kwa kufadhili mradi huu muhimu ni imani yetu kuwa malengo yaliyopangwa yatafikiwa na hivyo kuongeza upatikanaji wa masoko ya kimataifa na kuchochea uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja” amesema Mhe. Mavunde.

Amesema mradi huo umetokana na ukaguzi uliofanyika  nchini mwaka 2017 katika mifumo maalumu ya udhibiti wa mimea na mazao yanayosafirishwa kwenda nchi za jumuiya ya Ulaya na ukaguzi huo kubaini mapungufu ya afya ya mimea.

Aidha Mavunde ametaja baadhi ya maeneo yaliyobainika kuwa na mapungufu hadi kupelekea kuanzishwa kwa mradi huo ni maarifa madogo kwa wakaguzi kuhusu matakwa ya usafi wa mazao hayo,  kukosekana kwa mfumo kukusanya takwimu za visumbufu vya mimea, kukosekana kwa maabara zenye uwezo wa kufanya uchunguzi muhimu ili kuthibiti cheti cha usafi wa mimea.

“kufuatia kubainika kwa mapungufu hayo na gharama za kufanya biashara ya mazao kuwa juu serikali ilichukua hatua kwa kuunganisha majukumu ya TPRI na ya afya ya mimea na viwatilifu TPHPA ambacho kimekuwa ni chombo kinachotambilika kimataifa” ameeleza Mavunde.

Hata hivyo ameeleza kuwa  kuja kwa mradi huu utawezesha kufikia malengo ya kuhakikisha ukuaji wa sekta ya kilimo hapa nchini kwa asilimia 10 na mauzo ya mazao ya kilimo yanaongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 1.2 za sasa hadi kufikia Dola bilioni 5 ifikapo mwaka 2030.

Amesema Wizara ya Kilimo itasimamia utaratibu na kuongeza utekelezaji wa mradi huo na kutaka kamati ya kusimamia mradi huo na kumtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kuwasimamia wataalamu ili kazi zilizopangwa kwenye mradi zitekelezeke kwa wakati.

Awali Mwakilishi wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Obadia Nyagilo amesema mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha mika mitatu na nusu kwa kiasi cha Euro milioni 10.1 kwa ushirikiano ambapo Jumuiya ya umoja wa Ulaya itatoa Euro milioni 9.5, FAO itatoa Euro 350’000 na Tanzania itatoa EURO 250,000.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya mimea na Viwatilifu Tanzania  TPHPA Dkt. Efraim Njau amesema sekta ya kilimo ni muhimu sana ambapo imeajiri zaidi ya asilimia 67 ya watanzania na kuchangia takribani asilimia 29 ya pato la taifa.

Ametaja baadhi ya majukumu yanayofanywa na TPHPA ni kusimamia na kuratibu tasnia nzima ya viuatilifu, kudhibiti ubora, uagizaji, usambazaji na kuchagiza matumizi sahihi na usalama wa viuatilifu, kufanya uchambuzi wa athari ya visumbufu.

Ameongeza kuwa “matokeo tarajiwa ya mradi huo ni kuziongezea uwezo maabara za mamlaka kujenga, kukarabati na kuweka vifaa katika maabara za Mamlaka, kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa visumbufu na masalia ya viuatilifu katika mnyroro wa thamani ya uzalishaji wa mazao hususa ni yale mbogamboga na matunda” amesema Dkt. Njau.

Aidha amesema mradi utakuwa na kamati ambayo itaundwa na itawajibika kukutana na mara mbili kwa mwaka kupitia na kuhakikisha malengo ya mradi yanakwenda kama yalivyopangwa.

Nae Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani FAO Bi. Nyebenyi Tipo amesema mradi huo umelenga kuhakikisha usalama wa Chakula hasa kwa mazao yanayovuka mipaka kwa kuhakikisha yanakuwa na ubora na kuhakikisha usalama wa chakula na FAO watatoa ushirikiano kuhakikisha mradi huo unatekelezeka na unaleta tija kwa kukuza sekta ya kilimo na mazao ya hapa nchi kupata soko nje.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Kamati  ya Kudumu  ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji Dkt.Christine Ishengoma ,akitoa salamu za Kamati yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

MWAKILISHI wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya EU Bw.Cedric Merel,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani FAO Bi. Nyebenyi Tipo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya mimea na Viwatilifu Tanzania  TPHPA Dkt. Efraim Njau,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani)  wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

 Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde,akizindua mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor