Featured Kitaifa

SHAKA:RAIS SAMIA AMEWAUMBUA WALIOBEZA MIRADI YA KIMKAKATI

Written by mzalendoeditor

Katibu Wa Itikadi Na Uenezi CCM Ndg. Shaka Hamdu Shaka ,Wananchi na Baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakipita katika Njia ya Watembea kwa miguu Kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja jipya la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 89.02 na zaidi ya Sh. bilioni 75 zimepangwa kutumika.

………………………

Na Mwandishi Wetu,Pwani
 
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka amesema Chama hicho kinaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati inavyoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
 
Amesema hata baadhi ya watu waliokuwa wakibeza na kutoa kauli za kejeli kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo sasa wameumbuka.
 
Shaka ameyasema hayo leo Septemba 18, 2022 baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja jipya la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 89.02 na zaidi ya Sh. bilioni 75 zimepangwa kutumika.
 
Aidha amesema jambo la kufurahisha ni kwamba ujenzi wa daraja hilo unakwenda kuandika historia ya kuwa miongoni mwa miradi michache nchini iliyokamilika kabla ya muda uliopangwa.
 
“Wakati Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani kulikuwa na maneno mengi sana kuhusu daraja hili la Wami na si hili tu bali maneno yalikuwa mengi Rais Samia hataendeleza mirad hii ya kimkakati, wiki mbili zilizopita tulikuwa Mwanza, tumeona ujenzi wa daraja la Kigongo – Busisi unavyokwenda kwa kasi kuliko tunavyofikiria. Tumeona ujenzi wa meli MV. Mwanza unavyokwenda kwa kasi kuliko tunavyofikiria na leo niko hapa daraja la Wami nashuhudia kwa macho yangu, mikono yangu lakini ukisimama hapa ukiangalia kule mbele unaona namna gani ambavyo Pwani na Tanga inavyong’ara kupitia daraja hili,” amesema.
 
Aliongeza kuwa, fedha zote zimetoka kwa wakati na hivyo ukichukua asilimia 47 na asilimia 42.2 unapata asilimia 89.2 kati ya hizo kazi kubwa imefanyika katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi kadhaa ya Rais Samia Suluhu Hassan huku akieleza kwamba hapo ndipo unaona namna gani ambavyo Watanzania wananufaika na kodi zao kwa sababu fedha iliyotoka kwenye daraja hilo ni ya ndani.
 
“Hakuna fedha ya mjomba hakuna fedha ya msaada ni fedha ya watoka jasho wa Tanzania ndio imefanya kazi hii na mtaalamu  alikuwa ananiambia katika historia ya nchi yetu na mimi nimefuatilia iko hivyo, hili litakuwa daraja la kwanza kukamilika kabla ya wakati uliokadiriwa, daraja hili lilikadiriwa litumie miaka minne lakini tutalifungua kabla ya Novemba ambao tungetegemea kwamba ndio mwezi wa mwisho,” amesema.

Katibu Wa Itikadi Na Uenezi CCM Ndg. Shaka Hamdu Shaka ,Wananchi na Baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakipita katika Njia ya Watembea kwa miguu Kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja jipya la Wami ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 89.02 na zaidi ya Sh. bilioni 75 zimepangwa kutumika.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akiwa na viongozi, wana CCM na wataalamu wakipita juu ya Daraja la Wami mkoani Pwani alipotembelea ujenzi wa daraja hilo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na viongozi, wana CCM na wataalamu wakati alipotembelea ujenzi wa Daraja la Wami mkoani Pwani, jana. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).

About the author

mzalendoeditor