Featured Michezo

‘NI KWELI NIMEMSAIDIA ALLY KAMWE KUPATA AJIRA AZAM IWEJE LEO TENA NIWE MBAYA”-MANARA

Written by mzalendoeditor

Msemaji wa Yanga Haji Manara,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Septemba 18,2022 jijini Dodoma

……………………………………. 

Na Bolgas Odilo-DODOMA

HAJI Manara amesema kuwa  yeye amehusika kumsaidia mchambuzi Ally  Kamwe kupata ajira Azam iweje leo tena awe mbaya.

Hayo ameyasema leo Septemba 18,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ,Manara ambaye amesimamishwa miaka miwili na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  kujihusisha masuala ya soka amesema kuwa yeye hana tatizo na Kamwe sababu ni mdogo wake.

“Nimemsaidia lakini ananisema kwenye mitandao ya kijamii alafu nikae kimya mimi sio mnafiki kwanza dini yangu inanikataza yaani yeye awe na haki lakini yeye hataki kukosolewa mambo ya Januari kwanini ayalete leo,”amehoji  Manara

Amesema aliyoyasema Kamwe hayana ukweli wowote kwamba anazuia ajira yake Yanga na ameshangaa kumzungumzia vibaya katika interview.

“Anasema nilimkatalia salamu tulipokutana Zanzibar sasa ningewezaje kuwa mnafiki kwa mtu aliyenitukania binti yangu kwanza hata Mwenyezimungu hapendi ni dhambi,”amesema.

Aidha Manara amesema kuwa yeye hausiki kuzuia mchakato wa Yanga kupata Afisa Habari mpya kwani yeye bado amejiriwa na anakula mshahara wake vizuri.

“Mimi sizuii Afisa Habari mpya kuja Yanga,sijapata nguvu hiyo msinisingizie mimi bado nimeajiriwa Yanga nalipwa mshahara wangu vizuri,”amesema Manara.

Hata hivyo  amesema anaikubali adhabu ya kufungiwa miaka miwili na TFF  na  anaendelea kuitumikia huku akidai mambo mengine waachiwe kamati ya rufaa na wanasheria.

”Adhabu ya kufungiwa na TFF miaka miwili Manara nimekubali na ninaendelea kuitumikia na mengine waachiwe kamati ya rufaa na wanasheria.”amesema Manara

About the author

mzalendoeditor