Featured Kimataifa

TUNISIA YATANGAZA AMRI YA KIFUNGO CHA MIAKA 5 JELA KWA HABARI ZA UONGO

Written by mzalendoeditor

RAIS wa Tunisia Kais Saied ametanga adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela kwa mtu anayeeneza habari za uongo nchini humo.

Pia  Rais Saied amesema kuwa  amri hiyo  inaweza kuwa ya kifungo cha hadi miaka 10 jela ikiwa habari za uongo au uzushi itawalenga maafisa wa ngazi za juu. 

Kwa mujibu wa amri iliyotolewa yeyote atahesabika kuwa ametenda kosa hilo ikiwa atadhamiria kutumia vyombo vya mawasiliano kwa lengo la kutoa habari, kuieneza au kuchapisha habari za uongo. 

Mkuu wa chama cha waandishi habari nchini Tunisia Mahdi Jlassi amesema sheria hiyo ni pigo kubwa kwa uhuru wa vyombo vya habari kwenye nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. 

Tunisia ilikuwa miongoni mwa nchi zilizopiga hatua ndefu katika sekta ya vyombo vya habari huru tangu kufanyika kwa mapinduzi nchini humo mnamo mwaka 2011.

Shirika la habari la serikali, TAP mara kwa mara limekuwa linachapisha habari za kuikosoa serikali.

About the author

mzalendoeditor