Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui katika Ofisi Ndozo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Septemba 2022. Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili juu ya kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa yao katika sekta za uwekezaji, ujenzi na uboreshaji wa miundombinu, biashara, usafiri na uchukuzi, nishati, kilimo, uchumi wa blue, elimu na utamaduni. Pia wamejadili umuhimu wa kuwa na kamati za kitaifa kwa ajili ya ufuatiliaji wa masuala ya msingi ya utekelezaji yaliyokubaliwa wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Ufarasa mwezi Februari 2022, pamoja na masuala mengine ya ushirikiano baina ya nchi zao. Vilevile wamejadili juu ya mchango unaotolewa na serikali ya Ufaransa katika masuala ya ulinzi wa amani pamoja na nafasi ya tanzania katika kusimamia masuala ya ulinzi na amani kikanda hususan katika Nchi wanachama za Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC), Nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na katika Umoja wa Afrika (AU). |
Mhe. Balozi Mulamula akiagana na Mhe. Nabil Hajlaoui baada ya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Septemba 2022. |
Mazungumzo yakiendelea. |
Picha ya Pamoja, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (wa pili kulia), Mhe. Nabil Hajlaoui (wa pili kushoto) na maafisa waliombatana nao katika mazungumzo yao. |