Featured Kitaifa

AMBROS AKAMATWA NA MENO YA TEMBO,KARATU

Written by mzalendoeditor

Na. Abel Paul wa Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limesema kuwa tarehe 10.09.2022 muda wa 08:00 usiku huko Kijiji cha Endabashi tarafa ya Endabashi Wilaya ya Karatu Mkoa wa Arusha Jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata mmtu mmoja REGINALD AMBROS maarufu Amsi (42) mkulima mkazi wa Endabashi akiwa na vipande viwili vya Jino la Tembo ambavyo alikuwa amevifunga ndani ya boksi.

Akitoa taarifa hiyo leo tarehe 12 agosti kamanda wa Poloisi mkoa wa kamishina msaidizi wa Polisi ACP JUSTINE MASEJO amesema kuwa Jeshi hilo kufanikiwa kukamata mtuhumiwa mmoja kutokana na taarifa za wananchi wenye mapenzi mema na rasilimali za nchi ambazo zimekuwa zikiliingizia Pato taifa ikiwa ni Pamoja na fedha za kigeni.

Kamanda masejo amebainisha kuwa uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akijihusisha na matukio ya biashara haramu ya uuzaji wa nyara za serikali ambapo Jeshi la Polisi linaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo ilikupata mtandao mzima.

Kamanda Masejo katika hatua nyingine ameleza kuwa Jeshi hilo lilifanikiwa kukamata jumla ya lita 1480 za pombe haramu aina ya gongo, mitambo 80 ya kutengeneza Pombe hiyo Pamoja na watuhumiwa 62 ambao wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

JELA MIAKA 80 KWA KOSA LA UBAKAJI

Kamanda masejo Pia amewaambia waaandishi wa habari kuwa katika kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia katika mkoa wa Arusha Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwa kamata watuhumiwa wawili ambao ni PAUL HILONGA (60) mkazi wa Karatu kwa kosa la kubaka mwingine ni ERASTO SIAS 24 mkazi wa Qurus wilaya ya karatu kwa kosa lakubaka mtoto mwenye umri wa miaka 08 ambao kwa pamoja wote wamefungwa miaka 80 uku akibainisha kuwa mshitakiwa Paul Hilonga amefungwa kifungo cha miaka 50 jela na Erasto Sias amefungwa 30 jela.

Sambamba na hilo Kamanda Masejo amekutana na askari katika wilaya ya Karatu na kubainisha kuwa lazima tukubali ukweli kuwa kuna baadhi yetu tunaenda kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi ambapo amewaambia askari kuwa hato sita kuchukua hatua kwa askari wasio zingatia nidhamu haki weledi na uadilifu kwa atakaye Kwenda kinyume na mwendo mwema wa Jeshi la Polisi.

About the author

mzalendoeditor