Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AHUTUBIA JUBILEE YA MIAKA 50 YA UMOJA WA WANAWAKE WAKATOLIKI TANZANIA (WAWATA) JIJINI DAR ES SALAAM

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia bidhaa mbalimbali kwenye mabanda ya Maonesho ya Umoja wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) kutoka majimbo mbalimbali nchini mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa tarehe 11 Septemba, 2022 kwa ajili ya kushiriki Jubilee ya miaka 50 ya Jumuiya hiyo tangu kuanzishwa kwake. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono Wageni mbalimbali pamoja na Wanachama wa Umoja wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa tarehe 11 Septemba, 2022 kwa ajili ya Sherehe za Jubilee ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwake. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Maaskofu wa Majimbo mbalimbali ya Kanisa Katoliki wakati wa Jubilee ya miaka 50 ya Umoja wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA)  iliyofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam . 

Matukio mbalimbali katika Jubilee ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) iliyofanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Jubilee ya miaka 50 ya tangu kuanzishwa Umoja wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) katika Sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

About the author

mzalendoeditor