WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akigawa hundi kwa wananchi waliopisha maeneo yao kutekelezwa mradi huo wa maji
………………………….
Na Oscar Assenga,MKINGA.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewataka watendaji waliopata dhamana ya kusimamia mradi mkubwa wa maji wilayani Mkinga mkoani Tanga kuhakikisha wanafanya kazi hiyo waledi na ufanisi huku wakitambua kwamba wananchi wanauhitaji mkubwa huduma hiyo ya maji ambayo wameisubiri kwa kipindi cha muda mrefu.
Aweso aliyasema hayo wakati halfa ya utiliaji saini ya utekelezaji wa mradi huo kati ya Wizara ya Maji na Kampuni inayotekeleza mradi huo ya STC ambapo mradi wa Horohoro-Mkinga wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 35 iliyofanyika wilayani Mkinga na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa mkoa Tanga,wakuu Tanga,wakuu wilaya, wabunge na viongozi wengine akiwemo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Saimon Nkanyemka ambaye ni Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara Maji.
Alisema mkandarasi huyo ambaye amepata kazi hiyo sio mgeni kwenye kazi na alikwisha kutekeleza kwa ufanisi mkubwa mradi mkubwa wa maji Longido ambao ulikuwa na changamoto na Rais alitusifia kazi hiyo ulioifanya kule hivyo kuhakikisha kwamba ufanisi uliouonyesha uwe zaidi ya mara kumi kwa ubora.
” Ndugu Mkandarasi hapa huna kisingizio na moja ya miradi ya kipaumbele ni huu mradi leo sikupongezi nakupa pole maana hekeheka yake baada ya utiliaji saini mradi huu ni mkubwa hapa ni nyumbani na sikuzote ukipigana vita ugenini lazima nyumbani kuwe na amani “Alisema Waziri Aweso.
Alisema kwamba mradi huo mwenyrzi mungu akinijalia atakuja kufungua Rais Samia Suluhu atakwenda mwenyewe kuuzindua huo huku akieleza kwamba sehemu ambayo watu wana matatizo jibu lake ni kuhakikisha wanatoam matokeo yake yanaonekana na wananchi wanaondokana na changamoto hiyo.
Alisema kwamba hivi sasa wameshaiani mkataba na wamepata mkandarasi hivyo waandae wamlipe malipo ya awali na huu ni mradi wa usambazaji ongea na wenye viwanda wakupe Mabomba yote yanayohusika yamwage kazi ianze.
“Umeona heshima waliokupa watu wa Mkinga hapa hebu siku Maji yamfika itakuwaje tunaomba utuheshimishe sisi na Rais wetu Samia Suluhu huu ni moja ya miradi ya kupaumbele na ametupa nguvu itoshe kusema Rais Samia ndio Suluhu ya changamoto kwenye wilaya ya Mkinga na watanzania kwa ujumla”Alisema.
Waziri Aweso alisema kwamba kubwa katika mradi huo ni mkandarasi ahakikishe anafanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na Jamii ya wananchi wa wilaya ya Mkinga huku akieleza kwamba uwepo wasipofanya hivyo wanaweza kusababisha miradi kukwama badala yake washirikiane nao ili kutekeleza mradi huo kwa viwango.
Aidha Waziri huyo alimtaka mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba kuhakikisha wanasimamia miradi huku akimwambia mkandarasi ambaye ataleta ataleta ubabaishaji asicheke naye atakikisha wanachukuliwa hatua kali dhidi yao ikiwemo kuhakikisha anazindua miradi iliyopo mkoani humo na akibaini kuwepo kwa kasoro wachukue hatua.
Waziri Aweso alisema awali Wizara hiyo lilikuwa ya kero lazima hapa zimeliwa kiasi fulani huku akieleza Wizara ya maji haijaajiri vibaka hivyo wakandarasi hakikisheni mnatakeleza wajibu wenu ipasavyo ili kuwapatia wananchi maji.
Awali akizungumza Mwakilishi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Saimon Nkanyemka alisema jambo la kwanza ni kuwakabidhi wananchi ambao wameathiriwa na ujenzi wa bwawa la Parungu Kasera ambapo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mradi unapoathiriwa kwa kiasi kikubwa wanananchi wanahitaji la kufidiwa.
Saimon ambaye pia ni Mwanasheria wa Wizara ya Maji alisema kwamba Serikali ya Awamu ya sita imejiwekea mikakati ya kuhakikisha kila wilaya inakuwa na bwawa na wilaya ya Mkinga kuna bwawa la Parungu Kasera na litawaathiri wananchi 12 na hivyo wamelipwa milioni 70.6 ili waweze kupisha ujenzi wa bwawa hilo.
Naye kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba Mgumba alisema mradi kwamba wanamshukuru Rais Samia Suluhu kwa utekelezaji wake huko akieleza kwamba ilani ya CCM Kwa mkoa wa Tanga imetekelezwa kwa vitendo na kuendelea kuguswa na shida za wananchi wa mkoa huo.
Alisema ameshuhudi utiaji saini wa mkataba huo wa zaidi ya bilioni 35 hivyo wanamshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuwapelekea maji ya Tanga na kuyapeleka mkinga .
Alisema kwamba hakuishia Mkinga alisema shida ya maji upo Handeni,Pangani.Muhesa ameiziingia halamshsuri hugo zavmji kwrnur mradi wa mji 28 na ametenga Bilioni 190 kwa ajili ya kutatatua maji kwenye wilaya hizo tatu lakini wakasema kilindi ndio halmashaurti iliyopo mbali kuliko zote wanapeleka bilioni 200 kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji kutoa Morogoro kupelekwa Tanga katika wilaya hiyo ya Kilindi na tayari Bilioni 40 zimekwisha kuwekwa ajili ya awamu ya kwanza.
Mkurugenzi wa mamlaka za maji mijini,CPA Joyce Msilu kulia akisaini mkataba wa utiliaji saini ya utekelezaji wa mradi wa Horohoro-Mkinga wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 35 iliyofanyika wilayani Mkinga na mkandarasi anayetekeleza mradi huo kutoka kampuni ya STC kati ya Wizara ya Maji na Kampuni inayotekeleza mradi huo ya STC
Mwakilishi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Saimon Nkanyemka wa pili kulia mwenye koti jeusi akisaini mkataba utiliaji saini ya utekelezaji wa mradi huo kati ya Wizara ya Maji na Kampuni inayotekeleza mradi huo ya STC ambapo mradi wa Horohoro-Mkinga wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 35 iliyofanyika wilayani Mkinga
Mwakilishi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Saimon Nkanyemka kulia akisaini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo kati ya Wizara ya Maji na Kampuni inayotekeleza mradi huo ya STC ambapo mradi wa Horohoro-Mkinga wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 35 iliyofanyika wilayani Mkinga na mkandarasi anayetekeleza mradi huo kutoka kampuni ya STC
|
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akigawa hundi kwa wananchi waliopisha maeneo yao kutekelezwa mradi huo wa maji |
|
Mwakilishi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Saimon Nkanyemka kulia akisaini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo kati ya Wizara ya Maji na Kampuni inayotekeleza mradi huo ya STC ambapo mradi wa Horohoro-Mkinga wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 35 iliyofanyika wilayani Mkinga na mkandarasi anayetekeleza mradi huo kutoka kampuni ya STC |
MKUU wa Mkoa wa Tanga akizungumza jambo wakati wa halfa hiyo kulia ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye alikuwa mgeni rasmi kushuhudia utiliaji saini wa mikataba hiyo
|
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Mnyema akizungumza wakati wa halfa hiyo |
|
Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini Mkoa wa Tanga (Ruwasa) Mhandisi Upendo Omari akizungumza wakati wa halfa hiyo |