Na Eva Godwin,MZALENDO MBLOG
SIMBA SC kutoka Tanzania imeunguruma nchini Malawi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Big Bullets mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika inayopigwa kwenye uwanja wa Taifa Bingu, Malawi.
Mabao ya Simba yamefungwa kupitia kwa Moses Phiri aliyefunga bao la kwanza dakika ya 29 na Mshambuliaji John Bocco kufunga bao la pili dakika ya 83.
Timu hizo zitarudiana Septemba 17,mwaka huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.