Featured Michezo

YANGA YAANZA VYEMA LIGI YA MABINGWA AFRIKA,MAYELE APIGA HAT-TRICK

Written by mzalendoeditor

Na Odilo-Bolgas,MZALENDO BLOG

TIMU ya Yanga SC imeanza vyema katika kampeni za kuwania kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa baada ya kuwachapa mabao 4-0 wenyeji Zalan FC kutoka nchini Sudan Kusini mchezo wa  mkondo wa kwanza hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga walipata mabao ya yote manne kipindi cha pili mara baada ya kipindi cha kwanza timu zote kwenda mapumziko bila kufungana.

Mshambuliaji hatari kwa sasa Fiston Mayele amefunga hat-trick akifunga dakika 45,85 na 88 huku bao moja likifungwa na Fei Toto dakika ya 55

Yanga watarudiana na Zalan FC Septemba 16,2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa wakiwa kama wenyeji 

About the author

mzalendoeditor