Waziri wa Maji Juma Aweso akizungumza wakati wa uzinduzi akizindua bodi ya tisa ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Tanga (Tanga Uwasa) katika halfa iliyofanyika kwenye Mamlaka hiyo na kuhudhuria na viongozi mbalimbali ikiwemo kuwakabidhi vitendea kazi
………………………
Na Oscar Assenga,Tanga.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amezindua bodi mpya ya tisa ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji ya Tanga Uwasa huku akiwateua watumishi wawili wa Mamlaka ya Maji ya Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani na Dorah Killo kuwa wakurugenzi wa Mamlaka za Maji.
Uteuzi huo umefanywa leo na Waziri Aweso wakati akizindua bodi ya tisa ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Tanga (Tanga Uwasa) katika halfa iliyofanyika kwenye Mamlaka hiyo na kuhudhuria na viongozi mbalimbali.
Akizungumza kabla ya kutangaza uteuzi huo Waziri Aweso alisema kwamba watumishi hao wamekuwa wakifanya kazi nzuri ambapo wakiamsha hata usiku wamekuwa wakitoa kuwajibika kwa wananchi.
“Watumishi Mhandisi Rashid Shabani na Dorah Kilo hawa ni watumishi hodari na shupavu ambao wamekuwa wakifanya kazi zao kwa bidii kubwa hata ukimwamsha usiku ukimuambia kuna tatizo anafanya na nimeridhishwa na utendaji wao hivyo kuanzia leo nakuteua wewe na Dorah kuwa Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji” Alisema Waziri Aweso
Katika bodi hiyo mpya iliyoteuliwa na Waziri Aweso itaongozwa na Mwenyekiti wake Dkt Fungo Ally,Katibu wake Mhandisi Geofrey Hilly huku wajumbe wengine wa bodi hiyo ni Pili Manyema,Sipora Liana,Dkt George Lugomela.
Wajumbe wengine ni Geofrey Malenda, Mariam Abdallah, Deogratius Ruhinda,Hilda James na Abdurham Shiloow.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo Waziri Aweso alisema bodi hiyo ina kazi ya kufanya kuhakikisha miradi iliyoanzishwa na bodi iliyokwisha kuhakikisha mnaikamilika na kuja na miradi mipya ya kimkakati.
Alisema moja ya changamoto ya miradi ya mkoa wa Tanga ni midogo huku akitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji na kwa sasa hakuna visingizio kwa sababu amepata fedha Dola Milioni 500 ya kutekeleza miradi ya maji miji 28 nchini wao Tanga katika miji hiyo wana miji minne maji kutoka Mto Pangani yanakwenda Handeni, Korogwe,Muheza na Pangani Bilioni 19 sio jambo jepesi.
Alisema Mkinga kulikuwa na changamoto kubwa sana ya Maji lakini kesho historia inakwenda kuandikwa bilioni 40 Maji yanapelekwa kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji kwenye wilaya hiyo ambayo ilikuwa inakabiliwa kwa tatizo hilo kwa muda mrefu.
“Itoshe kusema kwamba Rais Samia Suluhu ni Suluhu ya changamoto ya matatizo ya watanzania tumpigie makofi mh Rais”Alisema.
Aliwataka bodi hiyo wakiona kuna maeneo ambayo kuna changamoto shirikianeni muweza kuona namna ya kuyapatia ufumbuzi ili kuweza kuhakikisha yanatatuliwa.
Aidha alisema katika mkoa wa Tanga kuna miradi 62 hatuna visingizio na ni ya kimkakati iliyopelekwa mkoani humo huku akimuomba Mkuu wa mkoa huo Omari Mgumba kama suala la fedha wao ndio wanadhama na watapeleka fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo lakini isije kuletwa stori mkandarasi hapana haja na hilo mtu hana uwezo aondolewe
Alisema wenye uwezo wapewe nafasi ya kufanya kazi huku akiwataka wahandisi wa maji kuhakikisha wanasimamia miradi na kuifuatilia inakuwaje mkuu wa wilaya mpaka anafika lakini wao hawajafika kukagua miradi ya maji wahandisi wa maji furaha yenu watu wapate maji.
Waziri huyo alisema kwamba Wizara ya maji kwa sasa inafanya tathimini kwenye ngazi za mikoa na wilaya na watumishi kwenye kada ya Wizara ya maji mtu ambaye anafanya kazi wataendelea kufanya kazi asiyeweza watamsaidia lakini niwaombeni wahandisi wa maji Lindeni nafasi zenu.
Waziri wa Maji Juma Aweso akizungumza wakati wa uzinduzi akizindua bodi ya tisa ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Tanga (Tanga Uwasa) katika halfa iliyofanyika kwenye Mamlaka hiyo na kuhudhuria na viongozi mbalimbali ikiwemo kuwakabidhi vitendea kazi |
MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akizungumza wakati wa halfa hiyo
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akizungmza wakati wa uzinduzi huo wa bodi |
Sehemu ya watumishi wa Tanga Uwasa wakimsikiliza Waziri Aweso
Sehemu ya watumishi wa Tanga Uwasa wakimsikiliza Waziri Aweso |
Sehemu ya watumishi wa Tanga Uwasa wakimsikiliza Waziri Aweso |
Sehemu ya watumishi wa Tanga Uwasa wakimsikiliza Waziri Aweso