Featured Kimataifa

MALKIA ELIZABETH AFARIKI DUNIA

Written by mzalendoeditor

Malkia Elizabeth wa Uingereza amefariki dunia muda mfupi uliopita wakati akipatiwa matibabu.

Malkia Elizabeth  alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa siku kadhaa sasa kutokana na afya yake kutetereka.

Habari kutoka makazi yake huko Balmoral huko Scotland zimeeleza kuwa, afya ya malkia ilibadilika ghafla leo Alhamisi Septemba 8,2022 na kulazimika familia yake kukutana kwa dharura.

Kutokana na kifo hicho, mtoto wa Malkia Elizabeth, Prince Charles sasa ndio atakuwa mfalme na anatarajiwa kurejea jijini London kesho, Ijumaa Septemba 9, 2022.

About the author

mzalendoeditor