Alifanya vizuri na kazi kadhaa ikiwemo Check and Balance, Mj, Complete me ,Move pamoja na Have Fun lakini hivi karibuni ameachia wimbo wake uitwao Iz going unaoendelea kufanya vizuri katika mahadhi ya Afro beat akiwa anawakilisha nchini Nigeria.
Bad Boy Timz ni moja kati ya msanii anayefanya vizuri nchini Nigeria huku akiwa anakuja vizuri zaidi kuliteka soko la muziki kimataifa zaidi.
Timz ana mpango wa kuachia kazi mpya hivi karibuni ikiwa imeambatana na zawadi nyingine kubwa zaidi kwa mashabiki zake kwa maelezo zaidi fuatilia ukurasa wake wa instagram pamoja na kufanya ku subscribe kupitia chaneli yake ya youtube.@badboytimz