Featured Kitaifa

RAIS SAMIA KUFUNGUA KIKAO KAZI CHA POLISI

Written by mzalendoeditor

NA.Abel Paul wa Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi Tanzania lingependa kuwajulisha kuwa katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) iliyopo Moshi mkoa wa Kilimanjaro maarufu (CCP) kutafanyika kikao kazi cha Maafisa Wakuu waandamizi wa Makao Makuu, Makamanda wa Polisi Mikoa na Vikosi, kitakacho fanyika siku tatu Moshi Kilimanjaro.

Akitoa taarifa hiyo msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP DAVID MISIME amesema Kikao kazi hicho kitaanza tarehe 30 Agosti hadi tarehe 01 Sepetemba 2022. Ambapo Kikao kazi hicho kitafunguliwa na Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 30 Agosti 2022.

Aidha SACP MISIME amesema kuwa Jeshi la Polisi kila mwaka hufanya kikao kama hicho kwa ajili ya kufanya tathimini ya utendaji wake kwa kipindi cha mwaka mmoja na kuona wapi Jeshi hilo limefanya vizuri na wapi halijafanya vizuri na sababu zake na kuweka mikakati mipya ya kutekeleza majukumu ya Jeshi la Polisi kwa ufanisi zaidi kwa mwaka unaofuata.

Misime amewaambia waandishi wa Habari kuwa maandalizi yote ya kikao kazi hicho yamekamilika kwa asilimia kubwa kama inavyo takiwa.

About the author

mzalendoeditor