Featured Kitaifa

ASKARI WATAKIWA KUTENDA HAKI KWA WANANCHI

Written by mzalendoeditor

Na.Abel Paul wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha

Kamishina wa operesheni na mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini CP AWADHI HAJI amewataka askari wa Jeshi la Polisi nchini kutenda haki kwa wananchi na kutoa huduma bora kwa wananchi wanao wahudumia ili kujenga Imani kwa wananchi juu ya Jeshi lao.

Kamishina Awadhi amesema hayo leo agosti 27 2022 wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani Arusha ambapo amewataka viongozi wa Jeshi la Polisi mkoani humo kusimamia vyema maelekezo ya mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ambayo aliyatoa mara tu alipopewadhamana na amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama kuliongoza Jeshi la Polisi nchini.

Aidha CP AWADHI alipata wasaa wa kutembelea kituo cha Polisi utalii na diplomasia mkoani humo ambapo amesema kuwa mkoa wa Arusha ni kitovu cha utalii hivyo amewataka askari kutoa huduma bora kwa watalii wanaofika nchini ili kuleta maana halisi ya Tanzania The Royal Tour ambayo ilizinduliwa mapema mwaka huu na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Sambamba na hilo amewataka askari kuto kuwa na muhari kwa waharifu na walewote wenye dhamira ya kuchafua taswira ya nchi.

About the author

mzalendoeditor