Featured Kitaifa

BILIONEA MWINGINE WA MADINI YA TANZANITE APATIKANA MERERANI, DKT BITEKO ASISITIZA SEKTA IKO SALAMA CHINI YA RAIS SAMIA 

Written by mzalendoeditor
Waziri wa madini Dkt Dotto Biteko akionyesha madini hayo yenye thamani ya shilingi bilioni 2.24.
……………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, MANYARA.
Serikali imenunua vipande vya madini mawili ya Tanzanite kutoka kwa mchimbaji mdogo Anselm Kawishe yenye thamani ya Bilioni 2.24 huku moja likiwa na kilogram 1.48 na lingine likiwa na kilogram 3.7.
Akiongea katika hafla ya ununuzi wa madini hayo waziri wa Madini Dkt Dotto Biteko alisema alisema kuwa sekta ya madini iko salama chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu ambapo anataka kuona wachimbaji  na wafanyabiashara wa madini wanaongozwa na utaratibu unaoeleweka, wanaoiua wanapokwenda lakini pia wanaofanya kazi kwa furaha.
Dkt Biteko alisema kuwa mfumo wa maisha wa kazi ya madini inaongozwa na vitu viwili ambayo ni uaminifu na kazi ambapo ni lazima wachimbaji wajue wanatawaliwa kwa utaratibu gani na wanafanya kazi kwa utaratibu gani na utaratibu huo uwe wa kudumu ambapo hata mafanikio yaliyopo hivi Sasa Kuna watu ambao wamefanya kazi hadi kufikia hapo 
Alieleza kutokana na biashara ya Tanzanite kuhamia katika mji wa Mererani Rais Samia ametoa fedha kwaajili ya ujenzi wa jengo la Tanzanite City ambapo jengo hilo likikamilika Mererani haitakuwa kama ilivyo hivi Sasa.
Sambamba na hayo pia alimpongeza mchimbaji huyo kwa mafanikio makubwa ambapo alisema mafanikio hayo yatasaidia kukuza sekta ya utalii ikiwa ni pamoja na kutengeneza ajira kwa watanzania wengine.
Katibu mkuu wa wizara ya madini Adolf Ndunguru alisema madini hayo ambayo serikali inayanunua yamezalishwa katika Leseni ya uchimbaji mdogo ambapo kipande cha kwanza kina kilogram 1.48 na Ina ubora wa hali ya juu(AB) yenye thamani ya shilingi milioni 713.8 na kipande cha pili Ina uzito wa kilogram 3.74 uboro wa kati (BC) yenye thamani ya shilingi bilioni 1.5
Alisema 2021/2022 tume ya madini ilikusanya shilingi bilioni 623 sawa na asilimia 55.8 ya malengo yaliyokuwa yamewekwa ambapo kwa mwaka 2022/2023 time ya madini imepewa lengo la kukusanya bilioni 822 sawa na wastani wa shilingi bilioni 8.5 kwa mwezi.
Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka alimpongeza mchimbaji Anselem Kavishe kwa jitihada alizofanya kupata madini hayo lakini pia kuimba serikali ku attengeneza barabara inayoendea kwenye machimbo ndani ya ukuta kwa kiwango cha kokoto ili wachimbaji waweze kwenda kwenye migodi yao salama na kurudi salama kwani barabara hiyo haipitiki na imekuwa chanzo cha ajali.
Naye mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere ameiomba serikali kuangalia ni jinsi gani wanaweza kutazama upya suala la kuwepo kwa majicho ya serikali ndani ya migodi (waangalizi wa serikali) kwani inawezekana waliondolewa kwa sababu maalum lakini ni muhimu wakawepo kwaajili ya kuwa na uhakika zaidi juu ya idadi halisi ya madini yaliyozalishwa katika migodi. 
Hata hivyo mchimbaji huyo Anselm Kawishe akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa alianza kutafuta Tanzanite mwaka 2004 ambapo 2012 alijiingiza moja kwa moja kwenye tasnia hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiweme vijana ambao akishirikiana nao na kuanzisha mgodi wao na mwaka huu mwanzoni walianza kupata mafanikio kwa mgodi wao kuanza kuzalisha kidogo kidogo na ilipofika mwezi wa tano ndipo walipopata vipande vikubwa viwili.
“Vipande hivyo ndo hivi tulivyoviuza siku ya leo na ninawasihi wachimbaji wenzangu wasife moyo  kwani sio kwamba ni mtu mmoja tuu ndiye atayepata bali tutapata wote kikubwa ni kufanya kazi bila kukata tamaa,”Alisema Bilionea Kawishe.
Waziri wa madini Dkt Dotto Biteko akiongea katika hafla ya ununuaji wa madini ya Tanzanite kutoka kwa mchimbaji Anselm Kawishe katika miji wa Mererani.
utiaji saini mkataba wa ununuzi kati ya  Bilionea Anselm Kawishe na serikali.
waziri wa madini Dkt Dotto Biteko akionyesha madini hayo yenye thamani ya shilingi bilioni 2.24.
Bilionea Anselm Kawishe akingea katika hafla ya ununuzi wa madini yake iliyofanyika katika mji wa Mererani.
bilioni Anselm Kawishe akishikilia cheki ya bilioni 2.24 aliyopewa na serikali baada ya kununua madini yake.

About the author

mzalendoeditor