Featured Michezo

LIVERPOOL YAFANYA MAUAJI YAICHAPA 9-0 BOURNEMOUTH

Written by mzalendoeditor

Liverpool wamefanya mauaji ya kutisha dhidi ya AFC Bournemouth kwa kuichapa mabao 9-0 mchezo wa Ligi Kuu ya England uliopigwa  Uwanja wa Anfield.

Ushindi huo mnono umeifanya Liverpool ifikie rekodi ya kushinda mabao mengi kwenye mechi moja katika Ligi Kuu ya England iliyowekwa na Man United dhidi ya Ipswich mwaka 1994, Southampton mwaka 2021 na Leicester City kwa hao hao The Saints mwaka uliotangulia.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Roberto Firmino na Luis Diaz mawili kila mmoja, Trent Alexander-Arnold, Harvey Elliott, Virgil van Dijk, Christopher Mepham aliyejifunga na Fabio Carvalho.

About the author

mzalendoeditor