Featured Kitaifa

TANZANIA NA IRAN ZAAHIDI KUONGEZA MAENEO MAPYA YA USHIRIKIANO

Written by mzalendoeditor
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimuaga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mhe. Hossein Amirabdollahian mara baada ya kumaliza mazungumzo katika ofisi za Wizara jijini Dodoma
………………………..
Tanzania na Iran zimekubaliana kuibua maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za biashara, kilimo, masoko, utalii, uwekezaji, afya, madini, nishati na utaalamu.
 
Hayo yamefikiwa wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mhe. Hossein Amirabdollahian yaliyofanyika jijini Dodoma tarehe 26 Agosti 2022.
 
Waziri Mulamula ameeleza kuwa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran nchini imekuja wakati muafaka ambapo, mataifa hayo mawili yenye uhusiano wa kihistoria yanatimiza miaka 40 tokea kuanzishwa kwa uhusianao wa kidiplomasia.
 
‘’Ziara hii inatupa muendelezo mzuri katika kuimarisha uhusiano wetu na kuangalia maeneo mapya ya kukubaliana kushirikiana” alisema Waziri Mulamula.
 
Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mhe. Hossein Amirabdollahian alieleza utayari wa nchi yake kushirikiana na Tanzania katika kubadilishana utaalamu na uzoefu katika sekta mbalimbali za maendeleo ili uhusiano uliopo ulete faida za kiuchumi kwa manufaa ya mataifa hayo mawili. 
 
“Tumefungua ukurasa mpya wa uhusiano wa kidiplomasia kwa mataifa yetu, hivyo naamini kupitia ziara hii kutapatikana mafanikio yanayoonekana kwa maslahi ya mataifa yetu. 
 
Mhe. Hossein Amirabdollahian yupo nchini kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 24 hadi 26 Agosti 2022  akiambatana na ujumbe wa Wafanyabiashara, Wamiliki wa Viwanda na Maafisa Waandamizi ambao pamoja na mambo mengine walishiriki kongamano la biashara lililofanyika Dar Es Salaam 
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mhe. Hossein Amirabdollahian katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 26 Agosti 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimkabidhi zawadi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mhe. Hossein Amirabdollahian katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 26 Agosti 2022.

Picha ya pamoja, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mhe. Hossein Amirabdollahian  pamoja na ujumbe waliombatana nao katika mazungumzo yao.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimuaga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mhe. Hossein Amirabdollahian mara baada ya kumaliza mazungumzo katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 26 Agosti 2022.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha mmoja wa mjumbe aliyeambatana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mhe. Hossein Amirabdollahian baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma tarehe 26 Agosti 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mhe. Hossein Amirabdollahian katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 26 Agosti 2022.

About the author

mzalendoeditor