Featured Michezo

SIMBA QUEENS YATINGA NUSU FAINALI KLABU BINGWA AFRIKA MASHARIKI

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Simba Queens imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya Wanawake Afrika Mashariki na Kati baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Yei Joint Stars ya Sudan Kusini katika mchezo wa Kundi B jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Vivian Aquino Corazone dakika ya 15, Philemena Abakah mawili, dakika ya 22 na 63 na Opa Clement dakika ya 32.
Simba inakamilisha pointi tisa baada ya kushinda mechi zake zote za Kundi B, 6-0 dhidi ya Garde Republicane ya Djibouti na 2-0 dhidi ya She Corporates ya Uganda na kutinga Nusu Fainali kama kinara wa Kundi.

About the author

mzalendoeditor