Na Fredy Mgunda, Iringa.
Mashabiki wa Yanga Mjini Mafinga wameifunga timu ya mashabiki wa Simba wa mjini Mafinga kwa goli moja bila katika mchezo wa Mafinga SENSABIKA festival uliofanyika katika uwanja wa Wambi Mafinga kwa lengo la kahamasisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa siku ya SENSA.
Mafinga SENSABIKA festival ilikuwa inamichezo mbalimbali kama mpira wa miguu kwa mechi kati ya boda boda na bajaji wa Mjini Mafinga ambapo bajaji walishinda goli mbili bila, watumishi wameshinda kwa penati nne kwa tatu dhidi ya viongozi wa halmashauri ya Mafinga Mji na uongozi wa wilaya ya Mufindi na asubuhi kulifanyika zoezi la mazoezi ya viungo ambayo yalikuwa na lengo la kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa siku ya SENSA.
Akizungumza wakati wa Mafinga SENSABIKA festival Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mji Cosato Chumi alisema kuwa wananchi wamejitokeza kwa wingi katika tamasha hilo na wamepata ujumbe wa umuhimu wa SENSA.
Chumi alisema kuwa wameamua kuiunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha wananchi wote wanajitokeza kuhesabiwa siku ya SENSA tarehe 23/8/2022 kwa lengo kubwa la kuisaidia kupanga bajeti ya maendeleo kwa wananchi wa maeneo husika.
Alisema kuwa matukio ya Mafinga SENSABIKA festival yalikuwa yanatoa ujumbe kwa wananchi umuhimu wa SENSA ya watu na makazi kwa ajili ya maendeleo ya taifa la Tanzania.
Alisema kuwa serikali ikijua idadi maalamu ya wananchi wa maeneo husika itasaidia serikali kutatua changamoto na kupeleka kupeleka maendeleo kulingana na idadi ya wananchi wa maeneo husika.
Chumi alimazia kusema kuwa faida ya SENSA hii ndio dira ya miaka kumi ya Taifa la Tanzania hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kuhesabiwa siku ya SENSA.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule alisema kuwa wameshakuwa wanatoa elimu mara kwa mara juu ya umuhimu wa kuhesabiwa siku ya tarehe 23/8/2022.
Mtambule alisema kuwa wananchi wa mji wa mafinga wamejitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Mafinga SENSABIKA festival ambalo limefanyika katika uwanja wa Wambi Mafinga Mjini.
Mtambule alimazia kwa kuwaomba wananchi wa wilaya ya Mufindi kujitokeza kwa wingi siku ya SENSA na kuwa tayari kuhesabiwa.
Na Fredy Mgunda, Iringa.