Featured Kitaifa

RC SENYAMULE AZINDUA NAMBA YA DHARURA KIPINDI CHA SENSA KWA WANANCHI WA DODOMA

Written by mzalendoeditor

Makarani pamoja na Wasimamizi wa Sensa wakiimba kwa pamoja huku wakinyanyua vishikwambi vyao Leo Agosti 17, 2022 walipotembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule.

…………………………

Na Eva Godwin-Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amezindua namba ya dharura kwa Mkoa wa Dodoma ambayo itatumika kwa Wananchi kutoa taarifa kipindi cha Sensa ya Watu na Makazi

Amezindua Namba hiyo Leo Agosti 17, 2022 ambapo amekutana na kufanya Mazungumzo na Makarani pamoja na Wakufunzi wa Sensa 2022 Wilayani Chamwino Jijini Dodoma.

Amesema Namba hizo zitatumika kwa Wananchi wa Dodoma kama kutakuwa na changamoto kwenye Mtaa, Kijiji na kitongoji unapo ishi utatmia namba hizo.

“Namba hii itatumika kwa Wananchi wa Mkoa wa Dodoma kutoa changamoto za mtaa wako katika kipindi cha Sensa Mfano kama karani alipaswa kupita katika kitongoji chako na hajaweza kupita namba hiyo itatumika kutoa taarifa kama hiyo na changamoto nyinginezo”,amesema

“Wananchi Mkoa wa Dodoma Msiwe na nidhamu ya huoga katika kutoa changamoto ambayo ni muhimu kuitoa ili kupatiwa msaada”. Amesema Senyamule

Ameongezea kwa kusisitiza Nidhamu kwa matumizi ya Sahihi ya lugha kwa kutumia Kiswahili chenye kueleweka kwa Makarani wote ili kuwezesha kupata taarifa sahihi kwa Wananchi.

Amesema Nidhamu ni kitu cha msingi ambacho kitasaidia Nchi yetu kupata taarifa sahihi na nidhamu hiyo ni kuzingatia lugha sahihi ambazo zinatumika kuzungumza na Wananchi pamoja na Muonekano mzuri wa kuaminika.

” Hatutegemei kutumia lugha ambayo haieleweki kwa wananchi, tumia lugha ambayo inaweza kueleweka na kutunza eshima na staha kwa yule unaeongea nae ambayo inamuondolea hofu wakati wa mazungumzo”, amesema

” Na Jitahidini namna ya kujenga mahusiano mazuri na yule ambae unaenda kumuuliza maswali vitu hivi ni vidogo lakini vinakutanya upate taarifa sahihi na taarifa ambayo sio sahihi kwaio
Watoeni hofu watu ambao mnaenda kuwahudumia kwasababu itawawawezesha watanzania kuwaamini na kupata taarifa sahihi”. Amesema Senyamule

Senyamule amesema Vifaa vya Tehama vitumike vizuri pamoja na kuzingatia muda ifikapo 23 Agosti, 2022

” Siku moja Kabla ya 23 Agosti, 2022 ni lazima mkatembelee maeneo yenu ya kazi ili ikifika siku yenyewe tusisikie uzembe wowote unaofanyika kwa Maaraani na ninajua kila Karani anajitambua ndio maana yupoa hapa

“Tunzeni vishikwambi vyenu isije kutokea kama Ngoswe, Vifaa vyenu tunza na vilindeni kwa Manufaa ya Taifa letu”. Amesema Senyamule

Naye Mratibu wa Sensa Wilaya ya Chamwino Bugumba Kassile amesema kwa Wilaya ya Chamwino Mafunzo hayo yalifanyika kitarafa ambapo ni Tarafa tatu (3) zilikuwepo ikujumuisha Makarani, Wakufunzi pamoja na Wasimamizi wa Sensa 1634.

“Tulikuwa na Tarafa tatu (3) kwa Wilaya yetu hii ya Chamwino na Makarani wote kwa ujumla wapo 396 na pia Wasimamizi wa Sensa, Makarani na Wakufunzi jumla ni 1634 na Kesho Agosti 18, 3022 tunatarajia kumaliza mafunzo haya ya Makarani wa Sensa kwa ngazi inayohusu Dodoso la Jamii”, amesema

“Zoezi hili la Mafunzo limeenda vizuri na Makarani wetu wamekwisha kamilika kwaajili ya kuanza kazi na tumaamini watafanya kazi kwa kuzingatia kanuni na sheria kama ilivyopangwa”

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza na makarani, wakufunzi wa sensa 2022 pamoja na kuzindua  namba ya dharura kwa Mkoa wa Dodoma ambayo itatumika kwa Wananchi kutoa taarifa kipindi cha Sensa ya Watu na Makazi hafla iliyofanyika leo Agosti 17,2022 Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuyamakizungumza kwenye Mkutano wa makarani, wakufunzi wa sensa 2022 

Mratibu wa Sensa Wilaya ya Chamwino Bugumba Kassile akitoa taarifa ya Wakufunzi wa Sensa tangu kuanza hadi kumalizika hiyo kesho Agosti 18,2022 wakati Mkuu wa Mkoa alipowatembelea  Makarani pamoja na Wakufunzi wa Sensa 2022 wilayani Chamwino Mkoani Dodoma

Makarani pamoja na Wasimamizi wa Sensa wakiimba kwa pamoja huku wakinyanyua vishikwambi vyao Leo Agosti 17, 2022 walipotembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule

About the author

mzalendoeditor