Featured Michezo

MAYELE AIPA NGAO YA JAMII YANGA,YAITULIZA SIMBA KWA MKAPA

Written by mzalendoeditor

 

MABINGWA wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara Timu ya Yanga imepindua meza baada ya kuongozwa bao mpaka kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya watani zao Simba mchezo wa Ngao ya Jamii ya kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu mechi iliyopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 15 likifungwa na Kiungo Mshambuliaji Pape Sakho akipokea  pasi Clatous Chama hadi mapumziko Simba walienda wakiwa wako mbele ya bao moja.

Kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko kwa kuwaingiza Bernard Morrison na Jesus Moloko mnamo dakika ya 49 Mshambuliaji hatari Fiston Mayele,aliisawazishia Ysnga akipokea pasi ya Khalid Aucho

Mayele tena alirudi nyavu mnamo dakika ya 80 baada ya kupokea pasi ya  Dickson Job na kuwanyanyua mashabiki wa Yanga.

Kwa ushindi huo Mayele ameipatia taji la kwanza la Ngao ya Jamii msimu wa 2022/23 baada ya mwaka jana kufunga bao moja na kuipa taji tena

About the author

mzalendoeditor