Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS AZINDUA NISHATI MBADALA YA MKAA

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizindua mitambo ya kisasa ya uchorongaji na uchimbaji madini ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yenye thamani ya shilingi bilioni 2.3 wakati wa hafla ya miaka 50 ya STAMICO iliofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse juu ya mitambo ya kisasa ya uchorongaji na uchimbaji madini ya Shirika hilo mara baada ya kuizindua wakati wa hafla ya miaka 50 ya STAMICO iliofanyika leo Agosti 12,202 jijini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,akizungumza na viongozi, wadau wa sekta ya madini, watumishi pamoja na wananchi mbalimbali waliohudhuria hafla ya miaka 50 ya STAMICO iliofanyika leo Agosti 12,2022 jijini  Dodoma.

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko,akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yaliyofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ,akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yaliyofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa  hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yaliyofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse,akitoa taarifa ya shirika hilo wakati wa  hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yaliyofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Seif Gulamali,akitoa pongezi kwa STAMICO wakati wa  hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yaliyofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango,(hayupo pichani) wakati wa hafla ya miaka 50 ya STAMICO iliofanyika leo Agosti 12,2022 jijini  Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizindua mkaa mbadala (Rafiki Briquettes) ulioanzishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakati wa hafla ya  maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yaliyofanyika leo Agosti 12,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Uwekezaji katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Lightness Mauki akipokea mfano wa hundi ya Sh bilioni 2.2 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo ikiwa ni gawio kwa Serikali iliyokabidhiwa jana jijini Dodoma wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya STAMICO. Anayeshuhudia katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dk Venance Mwasse.

…………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Philip Mpango,ameitaka Wizara ya Madini, STAMICO na NEMC kuongeza kasi ya ukaguzi wa migodi na midogo ili kubaini na kudhibiti uharibifu wa mazingira.

Makamu wa Rais amesema hayo leo  Agosti 12, 2022 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) 

 Amasema elimu ya kutosha inapaswa kutolewa juu ya madhara makubwa ya uchafuzi wa mazingira kwa maisha ya binadamu na viumbe vingine hai na uendelevu wa ikolojia.

“Bado kuna migodi haizingatii utunzaji wa mazingira wanaachia maji machafu yenye madini ya Zebaki kuingia kwenye vyanzo vya maji hivyo kuleta madhara kwa wananchi niwatake wizara husika ,STAMICO na NEMC kudhibiti jambo hili haraka kabla halijaleta matatizo makubwa”Amesema Dkt.Mpango
Aidha,Dkt Mpango ameitaka wizara ya Madini kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kuhakikisha wanaweka mazingira rafiki ya afya kwa wachimbaji wa madini na kuboresha vitendea kazi ili visilete madhara kwa wachimbaji.
Pia Makamu wa Rais ametoa rai kwa taasisi za fedha kuendeleza jitihada za kuweka masharti nafuu ya upatikanaji wa mikopo kwa wachimbaji wadogo na wa kati ili kuwasaidia kupata mitaji na zana za kisasa zitakazo wawezesha kuongeza tija, ajira na kufanya shughuli za uchimbaji kwa kutumia teknolojia rafiki na mazingira yanayowazunguka.
Makamu wa Rais amesema serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea na jitihada za kuboresha sekta ya Madini na kuhakikisha inakua kwa kasi kubwa, inatoa ajira kwa watanzania wengi zaidi na kuchangia zaidi katika pato la Taifa.

Kwa upande wake Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema  shirika la madini la taifa STAMICO linapaswa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kuongeza ushindani duniani na sio Tanzania pekee.

Aidha Waziri Biteko ameipongeza STAMICO kwa ubunifu wakati wa kukabiliana na changamoto za taratibu za manunuzi zilizokuwa zinajitokeza.

” Mageuzi makubwa yaliyofanyika ndani ya shirika hilo ndio yameleta mafanikiao ambapo zaidi ya ajira 700 zimezalishwa ndani ya mgodi wa Kiwira.”amesema Dk.Biteko

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo,ameitaka STAMICO kuongeza uzalishaji wa Mkaa mbadala na kusambaza kwa wananchi ili kutunza mazingira huku akizitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa STAMICO katika utunzaji wa mazingira.

”Nawaasa kuhakikisha uzalishaji wa mkaa huo unaongezeka ili watanzania waweze kutumia na kusaidia katika utunzaji mazingira.”amesema Dkt.Jafo

Awali akitoa taarifa ya maendeleo ya STAMICO Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo Dkt. Venance Mwasse,amesema shirika limefanikiwa kufufua mgodi wa Kiwira ambao ulikufa toka mwaka 2012 ambapo kwa sasa unaendelea nashughuli zake kama kawaida pamoja na kusaini mkataba wa kuuza makaa ya mawe elfu sitini yenye thamani ya shilingi bilioni nne.

”STAMICO inatarajia kununua mitambo kumi kwa ajili ya wachimbaji wadogo pamoja kuendelea kuwasaidia wachimbaji wenye mahitaji maalumu.”amesema Dkt.Mwasse

Aidha Dkt.Mwasse amesema licha ya kuwepo kwa mafanikio makubwa katika shirika hilo lakini bado zipo changamoto zinazowakabili ikiwemo uhaba wa wafanyakazi, taratibu za ununuzi wa umma bado sio rafiki kwa biashara.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema kuwa Mkoa wa Dodoma una Madini mengi sana hivyo ameliomba Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) katika kuhadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake wasaidie kutambua kiasi cha madani yaliyopo katika mkoa wa Dodoma

“Niwaombe STAMICO Dodoma ni mkoa ambao una madini mengi sana hivyo tunahitaji kujua ni kiasi gani ya madini tulionayo katika mkoa wetu kwani tumekuwa tukifanya tu makisio naamini Dodoma ina madini aina nyingi nafikiri kasoro tu madini ya Tanzanite”Amesema Senyamule
Shirika la Madini la Taifa STAMICO limesherekea miaka yake 50 tangu kuanzishwa kwake kwa kutoa gawio la shilingi bilioni 2.2 kwa serikali ikiwa ni sehemu ya faida yake.

About the author

mzalendoeditor