Featured Kitaifa

TET YAELEZA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZAKE NA MWELEKEO WA UTEKELEZAJI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023.

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba akizungumza na waandishiwa habari wakati akieleza Utekelezaji wa shughuli za TET na Mwelekeo wa Utekelezaji kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.

 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumisshi wa TET wakati akieleza Utekelezaji wa shughuli za TET na Mwelekeo wa Utekelezaji kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.

**********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Kwa mwaka wa fedha 2022/2023, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inaendelea  kukamilishakazi ya  usambazaji wa vitabu vya masomo mbalimbali ngazi ya Sekondari  na kukamilisha uandishi wa vitabu vya masomo yote ya Ufundi kidato cha I-IV na masomo ya ziada.

Katika kazi hii Serikali imetenga jumla ya shilingi Bilioni  4,238,569,340  kuwezesha uandishi na uchapaji wa vitabu vya kiada vya masomo haya kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu na wasio na mahitaji maalumu  kidato cha I-IV.

Ameyasema hayo leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba wakati akieleza Utekelezaji wa shughuli za TET na Mwelekeo wa Utekelezaji kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.

Amesema pamoja na kuandaa nakala  ngumu za vitabu, TET inatambua na kuzingatia umuhimu  wa matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji. Hivyo, vitabu vyote vimewekwa katika mkataba Mtandao inayopatikana katika tovuti ya www.tie.go.tz.

Aidha amesema kwa mwaka wa Fedha 2022/2023, TET inatarajia kuendelea kutoa mafunzo kazini kwa walimu na wasimamizi wengine wa utekelezaji wa mitaala ambapo jumla  ya shilingi  Bilioni 1,400,000,000 zimetengwa na  zimelenga kuwafikia jumla  ya walimu na wasimamizi wa utekelezaji wa mitaala 8,500.

Ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022,  Serikali ilitoa shilingi Bilioni 1,243,400,000 kwaajili ya kutoa  mafunzo kwa walimu, wathibiti  ubora wa shule ambao  jukumu  lao kubwa ni kufuatilia utekelezaji wa mitaala na wasimamizi wengine wa utekelezaji wa mitaala.

“Kwa kutumia fedha hizi, TET iliweza kutoa mafunzo kazini kwa jumla ya walimu 4,627 wa Elimu ya Awali,  Msingi na Sekondari. Mchanganuo wa walimu hawa ni;  Walimu 200 wa Elimu ya Awali, 2,779 wa  Elimu ya Msingi, 927 wa Masomo ya kilimo,  Ufundi,Biashara na Sayansi Kimu na 730 wa masomo ya sayansi na Hisabati Ngazi ya Sekondari Kidato  cha I-IV”. Ameeleza Dkt.Komba

About the author

mzalendoeditor