Featured Kitaifa

TMDA YATEKETEZA BIDHAA BANDIA ZENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 35.53 KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA

Written by mzalendoeditor

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Julai 29,2022 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Taasisi hiyo kwa Kipindi cha Mwaka 2021/22 na Matarajio kwa Mwaka 2022/23.

WAANDISHI wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo,wakati akizungumzia Mafanikio ya Taasisi hiyo kwa Kipindi cha Mwaka 2021/22 na Matarajio kwa Mwaka 2022/23 leo Julai 29,2022 jijini Dodoma.

 

.……………………………..

Na Eva Godwin-DODOMA

MAMLAKA ya dawa na vifaa tiba Nchini (TMDA) kwa kipindi cha mwaka mmoja 2021/22 imefanikiwa kuteketeza bidhaa za jumla ya tani elfu 35.54 zenye thamani ya shilingi billion 35.53 ambazo matumizi yake hayafai kutumika katika Jamii ili kulinda afya za Wananchi.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) Adam Fimbo wakati anatoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mafanikio ya taasisi kwa kipindi cha mwaka 2021/22 na matarajio kwa mwaka 2022/23 ambapo amesema taasisi hiyo iliendesha operasheni hiyo ili kuzuia bidhaa ambazo hazifai kutumika katika jamii.

“Katika Mwaka 2020-2021 kiasi na thamani ya bidhaa za dawa na vifaa tiba visivyofaa kwa matumizi ya binadamu zilizoteketezwa imeongezeka kutoka tani 14,704.80 zenye thamani ya Tzs 8.5 bilioni zilizoteketezwa mwaka 2020-2021 na kufikia jumla ya tani 35,547.47 zenye thamani ya takribani Tzs 35.53 bilioni “,amesema

“Hizi zinajumuisha bidhaa zilizotolewa taarifa na zile zilizokamatwa katika kaguzi mbalimbali kuongezeka kwa bidhaa zilizoteketezwa kutokana na kuimarisha ukaguzi na elimu kwa Umma inayosaidia wateja kutoa taarifa juu ya bidhaa zisizofaa kwa matumizi”.Amesema Fimbo

Hata hivyo amesema mipango ya taasisi hiyo katika mwaka wa fedha ikiwemo kuimarisha ukaguzi wa bidhaa ili kudhibiti bidhaa duni kutokuwepo sokoni pamoja na kuendeleza viwanda vinavyozalisha dawa na vifaa tiba hapa nchini.

“Mpango Mkakati wa Miaka mitano 2021-2026 wa kitaifa wa kupambana na tumbaku pamoja na mpango kazi wa miaka mitano wa udhibiti wa tumbaku ambao umeanza kutekelezwa. Na tumeweka tayari mfumo wa udhibiti wa bidhaa hizi na hadi sasa tumekwishatambua bidhaa zote za tumbaku zilizoko kwenye soko ambapo idadi yake hadi sasa ni bidhaa 51.

“Aidha Mamlaka imeanzisha maabara ya upimaji wa bidhaa za tumbaku kwenye jengo lake lililomo hapa Dodoma.
Mamlaka imeweka mfumo madhubuti wa ufuatikiaji wa Madhara yatokanayo na matumizi ya dawa, chanjo na vifaa tiba ilikuweza kubaini, kutathmini na kuzuia madhara yasiyovumilika yasitokee kwa Wananchi”.Amesema Fimbo

Ameongezea kwa kusema Mafanikio haya ya TMDA yametokana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya sita

“Ni dhahiri kuwa mafanikio yaliyofikiwa na TMDA yametokana na Dhamira ya Serikali ya Awamu ya sita Nchini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

“hii ni kuhakikisha kuwa Wananchi wanapata dawa,Vifaa tiba vitendanishi na chanjo zilizo bora, salama na Fanisi”.Amesema

About the author

mzalendoeditor