Featured Kitaifa

SHAKA:”KINANA NI CHUO KIKUU CHA SIASA KINACHOTEMBEA’

Written by mzalendoeditor


Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Mbeya

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka amesema kwamba Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana ni Chuo kikuu cha siasa kinachotembea.

Shaka ameyasema hayo leo Julai 29,2022 wakati akizungumza kwenye mkutano wa ndani uliohusisha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Mbeya ambapo ametumia nafasi hiyo kuelezea uwezo wa Kinana katika medani ya siasa ndani na nje ya Tanzania.

“Leo nina utambulisho maalumu kwa wana Mbeya ukingalinganisha na huko ambako tumepita, tulianza ziara tarehe 25 kwa kuanza na Mkoa wa Katavi, tukaenda Rukwa, Songwe na leo tuko Mbeya.

“Nawashukuru sana , kwanza namshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Kinana kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, wajumbe wa mkutano mkuu nawashukuru kwa kumpitisha Kinana.Kabla sijafanya huo utambulisho amekulia ndani ya TANU na hatimaye CCM.

“Kinana ni gwiji la siasa wa siasa za ndani na nje ya Tanzania.Kinana ni Chuo kikuu cha siasa ambacho kinatembea, wanaCCM hasa vijana tunakila sababu ya kujifunza kupitia yeye, tutembee katika nyazo zake,”amesema.

Shaka baada ya kutoa maelezo hayo kuwezo uwezo wa Kinana katika medani ya siasa ametumia nafasi hiyo kuwatambulisha rasmi wana CCM Mkoa wa Mbeya kwamba Kinana ndio mlezi wa mkoa huo.

“Kinana ndio mlezi wa Mkoa wa Mbeya, uzuri wa Chama chetu ulezi wetu sio wa kuchapana fimbo, ni ulezi wa kushauriana na kupeana mawazo ya kujenga Chama,amesema Shaka.

Katika hatua nyingine Shaka amesema kwamba kazi kubwa na nzuri ambayo inafanywa na Rais Samia katika kuwatumikia Watanzania wakiwemo wa mkoa wa Mbeya ni ukweli anaufuta upinzani.

“Kwa waliosoma shule wanajua kufuta kwa ufutio lakini Rais Samia anaufuta upinzani kwa kuleta maendeleo, hivyo kazi kwenu wana Mbeya ifikapo mwaka 20225.

Katibu wa Halmashuri Kuu ya Taifa,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM,Ndugu Shaka Hamdu Shaka akizungumza ndani ya ukumbi wa Ben Mkapa wakati wa mkutano wa ndani uliohusisha Wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mbeya leo Julai 28,2028,ambapo amemtambulisha Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana kuwa ndiye mlezi wa Mkoa wa Mbeya.PICHA NA MICHUZI JR-MBEYA.

Katibu wa Halmashuri Kuu ya Taifa,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM,Ndugu Shaka Hamdu Shaka akifurahia jambo na  Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana mara baada ya kutambulishwa rasmi kuwa kuwa ndiye mlezi wa Mkoa wa Mbeya.

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakifurahia baada ya Katibu wa Halmashuri Kuu ya Taifa,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM,Ndugu Shaka Hamdu Shaka kumtambulisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndugu Abdulrahman Kinana kuwa ndiye Mlezi wa Mkoa huo
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya ukumbi huo.


Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakifurahia baada ya kufanyika utambulisho maalum wa kumtaja Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndugu Abdulrahman Kinana kuwa ndiye Mlezi wa Mkoa huo.PICHA NA MICHUZI JR-MBEYA.

About the author

mzalendoeditor