Na John Mapepele, Birmingham
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa ameitembelea
timu ya wachezaji wa Tanzania inayoshiriki mashindano ya Jumuiya ya
Madola   Birmingham nchini Uingereza na kuitaka kupambana kufa na kupona
ili kurejea na medali.
Mhe.
Mchengerwa ameyasema haya leo Julai 27, 2022 kwenye kambi ya timu hiyo
huku akisisitiza kuwa watanzania wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan wana matumaini makubwa na
timu hiyo hivyo hawana budi kulinda heshima kubwa waliyopewa na taifa
kwa ujumla.
“Nawaomba
tangulizeni uzalendo ili tuweze kushinda, hii ni vita  tunahitaji
kupambana bila kujali idadi yetu wala kitu chochote. Tutashinda.”
Amesisitiza Mhe. Mchengerwa
Aidha, 
amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuinua  na kuendeleza michezo
kwa kuwa michezo ni chanzo. Ha ajira na uchumi kwa taifa

kwa kutambua hilo ndiyo maana kwa mara ya kwanza Serikali  imeamua
kutoa fedha nyingi kwa wachezaji watakaopata medali za dhahabu dola za
kimarekani 10,000, shaba 7500 na fedha 5000 bado zawadi za jumla”
amesisitiza  Mhe. Mchengerwa.
Pia
ametumia tukio hilo kutoa pongezi kwa timu ya wanaume na wanawake ya
KABBADI kwa kufuzu kuingia kwenye mashindano ya kombe la Dunia
yatakayofanyika Oktoba mwaka huu nchini India.
Mhe
Mchengerwa ameongozana na Mhe. Musa Sima Mjumbe wa Kamati ya Bunge
inayosimamia wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na ndugu Saidi Yakubu
Naibu Katibu Mkuu.
Previous articleWAZIRI MAKAMBA:’MRADI MKUBWA WA KUSAFIRISHA UMEME WA TANZANIA-ZAMBIA KUKAMILIKA JANUARI 2025′
Next articleMKE WA RAIS WA ZANZIBAR AONGOZA MATEMBEZI NA MAZOEZI YA VIUNGO KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA WETE PEMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here