Featured Kitaifa

MAJALIWA AITISHA KIKAO KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA KUTAFUTA ENEO UTAKAPOJENGWA MNARA WA MASHUJAA

Written by mzalendoeditor

WAZIRI  Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 25, 2022 ameitisha kikao cha kujadili utelekezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa jijini Dodoma la kuitaka Ofisi ya Waziri Mkuu itafute eneo jingine utakapojengwa mnara mpya wa mashujaa wenye hadhi ya Makao Makuu ya nchi. 

Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akiongoza kikao hicho kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,  Bunge na Uratibu, George Simbachawene na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

About the author

mzalendoeditor