Featured Kitaifa

RAIS SAMIA MGENI RASMI SIKU YA MASHUJAA DODOMA

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka, akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 21,2022 jijini Dodoma mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maandalizi ya Siku ya Mashujaa Kitaifa yatafanyika Julai 25,2022 jijini Dodoma na Mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan. 

Mkurugenzi wa Maadhimisho ya taifa Ofisi ya Waziri Mkuu, Batholomeo Jungu,akielezea maandalizi ya Siku ya Mashujaa yatakayofanyika Julai 25,2022 jijini Dodoma na Mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan. 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka, akikagua  maandalizi ya Siku ya Mashujaa yatakayofanyika  Julai 25,2022 jijini Dodoma na Mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan. 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Fatma Maganga mara baada ya  kukagua maandalizi ya Siku ya Mashujaa yatakayofanyika Julai 25,2022 jijini Dodoma na Mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan. 

…………………………………………………

Na Eva Godwin-DODOMA

RAIS Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa kitaifa itakayo adhimishwa jijini Dodoma Julai 25, 2022.

Hayo yamesemwa leo Julai 21,2022 jijini Dodoma na  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati akizungumza na Waandishi wa habari .

Amesema Wakazi wa Dodoma wajiandae kujumuika katika kushiriki siku ya sherehe ya Mashujaa ambapo pia Sherehe hiyo itaongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Sherehe za mashujaa kitaifa zinafanyika Dodoma na Rais samia atakuwa Mgeni rasmi siku hiyo tujiandae kujumuika na Rais wetu kwenye siku hiyo Muhimu”,amesema

“Hii ni heshima kubwa sana kwetu wanadodoma siku ya mashujaa kitaifa kufanyika Jijini Dodoma na sisi Mkoa tumejiandaa vizuri katika siku hiyo”.Amesema Mtaka

Ameongezea kwakusema tarehe 24 Julai,2022 Saa sita kamili usiku amewataka Wananchi kwa kushirikiana na viongozi wa Mkoa kufika katika uwanja wa mashujaa wakati wa tukio la uwashaji wa Mwenge.

“Niwaalike Wananchi wote siku ya tarehe 24 Julai, 2022 tufike katika viwanja vya mashujaa kwaajili ya kuwasha mwenge na na sisi viongozi wa Mkoa tunaendelea na maandalizi mpaka kufikia siku hiyo”,amesema

“Mimi nitawaongoza katika tukio hilo la uwashaji wa Mwenge na tarehe 25 Julai 2022 Saa sita usiku Mwenge utazimwa na Mstahiki Meya Profesa David Mwamfupe”.Amesema Mtaka

About the author

mzalendoeditor