Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA 22 WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC) JIJINI ARUSHA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha AICC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulionza tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Wawakilishi wakati wa Wimbo wa Taifa wa Afrika Mashariki ukipigwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa AICC Jijini Arusha kabla ya kuanza kwa Kikao cha Wakuu hao wa Nchi tarehe 21 Julai, 2022.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza  na Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha AICC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulionza tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Arusha.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza  na Rais wa Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC Jijini Arusha

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulionza tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Arusha

About the author

mzalendoeditor