Afisa Usalama wa Shirika la Tanesco Mkoa wa Tanga Emanuel Kimario akizungumza na waandishi wa habari leo . |
Afisa Usalama wa Shirika la Tanesco Mkoa wa Tanga Emanuel Kimario akizungumza na waandishi wa habari leo .
Na Oscar Assenga, Tanga
SHIRIKA
la Umeme nchini Tanesco limewaonya wananchi wenye tabia za kuhujumu
miundombinu kuacha mara moja tabia hizo kabla hawajachukuliwa hatua kali
za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani na kifungo.
Onyo hilo
lilitolewa na Afisa Usalama wa Shirika la Tanesco Mkoa wa Tanga Emanuel
Kimario wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu
changamoto zinazosababisha ukosefu wa umeme kutokana na uharibifu na
hujuma kwenye miundombinu ya shirika hilo.
Alisema vitendo hivyo
vinafanywa na baadhi ya wananchi wasio waaminifu na kusababisha shirika
kutumua fedha nyingi kurudisha huduma na shughuli za umeme katika hali
ya kawaida na pia kupelekea wateja kukosa huduma hiyo na kuzorotesha
shughuli za kiuchumi za kila siku.
“Lakini kutokana na gharama
kubwa ambazo zinatumika kurudisha huduma kutokana na uharibifu shirika
linaingia gharama kubwa na hivyo kupunguza kasi ya usambazaji wa umeme
kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na umeme”alisema
Hata hivyo
aliomba wananchi wawape ushirikiano kwa kuwafuchua wananchi ambao
wamekuwa wakihujumu miundombinu ya shirika hilo ikiwemo kutoa taarifa
kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili waweze kuchukuliwa hatua na
kuhakikisha miundombinu yao inakuwa salama na huduma inapatikana
ipasavyo.
“Tumekuwa tukifanya operesheni kwa kushirikiana na
vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha huduma inapatikana na pale
ambapo mwananchi anabainika amehujumu miundombinu kunawachukuliwa
hatua”Alisema
Aidha alisema hivi karibu kwa kushirikiana na
vyombo vya ulinzi na usalama kulitokea hujuma kwenye maeneo yao na
walifanikiwa kuwamata baadhi ya watuhumiwa mashauri yao yapo mahakamani
na mmoja wapo alifunguliwa shauri la uhujumu uchumi namba 1 la mwaka
2022 na limemalizika na mtuhumiwa amehukumiwa kwenda Jela miaka 20.
Alisema hatua ya kukamatwa
mtuhumiwa huyo na wengine ambao mashauri saba yanaendelea kwenye
mahakama za wilaya za Handeni,Lushoto na Tanga mjini ambapo kati ya hayo mawili yametolewa hukumu ni
kutokana na operesheni ambayo wameifanya kushirikiana na vyombo vyengine vya
usalama na kufanikiwa kuwakamataa.
Alimtaja
mtuhumiwa huyo kuwa Mahamud Hamisi shauri hilo lilimalizika Julai 12
mwaka huu huku akitoa rai kwa wananchi kulinda miundombinu na kuitunza
ikiwemo kutambua kwamba ni jukumu la watu wote kuilinda na wale
wanaofanya hujuma kuacha kufanya hivyo kwani hawapo tayari kuona watu
wachache wanahujumu muindimbiu hiyo .