Featured Kitaifa

RAIS WA TAASISI YA KOFIH PROF.KIM ATEMBELEA OFISI YA MKUU WA DODOMA NA WILAYA YA KONGWA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Taasisi ya Korea Foundation for International Healthcare ( KOFIH) Professor Kim ametembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma pomoja na Halmashauri ya Wilaya Kongwa.

Profesa Kim pamoja na ujumbe wake wamefanya ziara hiyo ili kujionea utoaji wa huduma za afya ikiwa ni pamoja na kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Kongwa.

KOFIH kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma wanatekeleza Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto katika Halmashauri za Kongwa na Mpwapwa.

Ili kutekeleza adhma hiyo Taasisi ya KOFIH imetoa fedha kwa ajili ya kusaidia Hospital ya Wilaya ya Kongwa katika ununuzi wa vifaa tiba vikiwepo Mashine 2 za usingizi, vifaa vya Maabara na vifaa vya kujikinga na maambukizi. Kiasi cha fedha ambazo KOFIH imetoa kwa ajili ya Hospitali ya Kongwa ni Tsh. 186,000,000/-.

Aidha, Taasisi ya KOFIH imetoa kiasi cha Tsh. 460,000,000/- kwa ajili ya Uboreshaji wa Miundombinu ya Vituo vya Afya vya Chamkoroma (Kongwa) na Rudi (Mpwapwa). Vilevile Taasisi hiyo imekwishatoa kiasi cha Tsh. 204,000,000/- kwa ajili ya ununuzi wa Mashine ya Mionzi ya Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa.

Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH ) ni Shirika la Serikali ya Korea ambalo linatoa msaada katika utoaji wa Huduma za Afya Duniani.

Mradi KOFIH nchini Tanzania ni wa miaka mitano 2021/2026 ambao unahusisha Uboreshaji wa Miundombinu katika Vituo vya Kutolea Huduma za Afya ili kuwezesha utoaji wa Huduma za dharura za Upasuaji, ununuzi na uwekaji wa vifaa tiba kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa Huduma bora za Afya, utoaji wa mafunzo mbalimbali kwa watumishi wa Afya Ili kuwajengea uwezo na kuwawezesha kutoa huduma bora za Afya pamoja na kuiwezesha Jamii kuongeza ushiriki wao katika utoaji na upokeaji wa Huduma za afya. MWISHO

About the author

mzalendoeditor