Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE WA ZAMANI WA CUF

Written by mzalendoeditor

CHAMA Cha Mapinduzi @ccmtanzania Kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa zamani wa Chama Cha Wananchi (CUF) na Mkurugenzi wa Fedha na Mipango Bi Khadija Makontena kilichotokea Alhamisi 14 Julai, 2022.

Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu  Hassan amemtumia salaam za pole Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF ) Profesa Ibrahim Lipumba, familia, ndugu na jamaa.

“Bi Khadija tokea kuanzishwa mfumo  wa Vyama Vingi vya siasa amekuwa akishiriki kikamilifu  katika uwanja wa  siasa za ndani na nje ya  chama chake huku  akiamini   siasa za umoja na maelewano.” Ndugu Samia Suluhu Hassan

Mwenyezi Mungu awape ustahamilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Sisi Sote niwa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.

Shaka Hamdu Shaka
Katibu Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
14 Julai, 2022

About the author

mzalendoeditor