WAKILI Peter Michael Madeleka akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama mara baada ya kumalizika kusikilizwa kwa maombi yake dhidi ya Jamuhuri
…………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha inatarajia kutoa maamuzi ya maombi madogo ya jinai namba 1/2022 yaliyotolewa na Peter Michael Madeleka dhidi ya Jamhuri ya kumuondoa hatiani Julai 29,2022 kutokana na hukumu ya kesi ya ujuhumu uchumi namba 40/2020 baada ya kusikilizwa Julai 13, 2022.
Maombi hayo yalisikilizwa na Hakimu Herieth Mhenga upande wa muombaji wakili Peter Madeleka alieleza kuwa hukumu hiyo haukufuata sheria kutokana na fedha za prebagein kulipwa kwa DPP badala ya kulipwa hazina.
“Lakini kosa nililohukumiwa nalo halikuwa kosa la uhujumu uchumi nililoshtakiwa nalo tangu awali bali ni kosa ambalo nililiona kwa mara ya kwanza siku ambayo nilipelekwa mahakamani pamoja na pesa ambazo nilimlipa DPP machi 30,2021 nililipa takribani mwezi mzima kabla ya kufikia makubaliano tuliyoyafanya mahakamani nililipa nikiwa Gerezani na hakuwa na namna nyingine yoyote,” Alisema
Kwa upande wake Wakili mwandamizi wa serikali Akisa Mhando alisema kwa mujibu wa vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo katika fedha ya uhujumu uchumi namba 40/2020 ya utakatishaji fedha iliyokuwa ikimkabili wakili Peter Madeleka inaonyesha kwamba yeye mwenyewe ndiye aliyeandika barua ya kuomba pribageini.
“Barua hiyo aliiandika bila kushawishiwa akiwa na akili zake timamu hivyo naiomba mahakama isibadilishe kitu chochote kutokana na barua hiyo kuandika wakili Peter Madeleka lakini pia inaonyesha Peter Madeleka alileta risiti za malipo ya milioni mbili katika mahakama lakini pia baada ya hapo hoja zilisomwa mahakamani na Peter Madeleka alikuwa na nafasi ya kupinga hoja hizo lakini hakupinga ikiwa hoja hiyo ilisomwa kwa lugha anayoielewa,” Alisema.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo wakili Peter Madeleka alisema shauri hilo limesikilizwa katika mahakama hiyo na hoja kubwa ni kulingana na makubaliano ya mwendesha mashtaka na yeye ambayo alimuamuru alipe pesa kama fidia kiasi cha shilingi milioni 2 huku kwa mujibu wa kanuni ya pre bagein DPP haruhusiwi kupokea fedha kutoka kwa mtuhumiwa.
Alisema kwa kanuni za kisheria zinazosimamia pribageini DPP hapaswi kupokea fedha kutoka kwa mtuhumiwa hata kama kuna makubaliano na isitoshe kama fidia zitakuwa zikilipwa kwa serikali anayepaswa kuzipokea ni msajili wa hazina na hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 21 ndogo ya 3A ya pribageini.
“Kitendo hicho kinafanya kesi nzima, hukumu pamoja na adhabu ziweze kuwa ni batili kwa sababu hukumu yote ya mahakama na mwenendo wote wa kesi ili iweze kuwa halali lazima izingatie sheria, tunasubiri maamuzi ya mahakama na nitapokea maamuzi na kama kutakuwa na haja ya kuendelea na kesi hii nitaenda katika hatua nyingine,” Alisema.