Burudani Featured

WAZIRI MCHENGERWA KUUNDA KAMATI MAALUMU YA KUANDAA MDUNDOWA KITANZANIA

Written by mzalendoeditor

Na John Mapepele
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema
anakwenda kuunda kamati maalum kwa ajili ya kuratibu uzalishaji mdundo 
wa muziki wa  kitanzania ambao utaitangaza  Tanzania Duniani.  
Mhe.
Mchengerwa ameyasema hayo leo Julai 13, 2022 alipotembelea studio ya
kuzalisha kazi za sanaa ya Wanene na kufanya majadiliano na wafanyakazi
wa studio hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
 “Dhamira
ya Serikali kwa sasa ni kuwa na mdundo utakaoitambulisha nchi yetu
kimataifa ili kuuza utamaduni wa nchi yetu kwenye mataifa mbalimbali
duniani” amesisitiza Mhe. Mchengerwa.
Amesema
Kamati hiyo maalum itaundwa na walimu wabobezi   kutoka vyuo vikuu,
wazalishaji wa Muziki, wanamuziki pamoja na viongozi wa kimila(machifu).
Amesema
Tanzania imebahatika kuwa na utajiri wa utamaduni ambao kama utatumika
vizuri kutengeneza midundo  ya miziki kama ilivyo kwa nchi mbalimbali
duniani utasaidia  kuitangaza  Tanzania na  kuinua  uchumi wa Tanzania.
Aidha,
amewapongeza wazalishaji hao wa muziki ambapo amesema wanafanya kazi
nzuri ya  kuandaa kazi bora  ambazo zina ubunifu mkubwa. 
Amesema
amefurahishwa kuona wazalishaji wenye ubunifu mkubwa ambapo
amesisistiza kuwa kama watashirikiana kwa pamoja na Serikali wataweza
Kwa upande wake Meneja wa Studio ya Wanene Humphrey Domboka amemshukuru
Waziri Mchengerwa kwa kuwa karibu na wadau wa wa sekta ambazo
anazisimamia.
Domboka
amesema endapo Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi
kunakuwa na mapinduzi makubwa ambapo amempongeza Mhe. Rais kwa kazi
kubwa anayofanya  kwenye sekta ya Sanaa, Utamaduni na Michezo.

About the author

mzalendoeditor