Featured Kitaifa

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS OTHMAN MASOUD AFUNGUA KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA MAISHA YA HAYATI BENJAMINI MKAPA

Written by mzalendoeditor

Makamo wa kwanza wa Rais  Mhe.Othman Massoud Othman akiaangalia bidhaa katika baadhi ya mabanda alipofika Hoteli ya Golden Tulip  Uwanja wa Ndege Zanzibar Kufungua kongamano la kumbukizi ya maisha ya Rais wa Awamu ya tatu ambae pia ni muasisi na msarifu wa Tassisi ya Benjamin Mkapa Foundation (BMF) Hayati  Benjamin William Mkapa. Makamo wa kwanza wa Rais  Mhe.Othman Massoud Othman akizungumza wakati akifungua kongamano la kumbukizi ya maisha ya Rais wa Awamu ya tatu ambae pia ni muasisi na msarifu wa Tassisi ya Benjamin Mkapa Foundation (BMF) Hayati  Benjamin William Mkapa lililofanyika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip  Uwanja wa Ndege Zanzibar. 

Viongozi mbalimbali SMZ NA SMT wakifuatilia hafla ya kongamano la kumbukizi ya maisha ya Rais wa Awamu ya tatu ambae pia ni muasisi na msarifu wa Tassisi ya Benjamin Mkapa Foundation (BMF) Hayati  Benjamin William Mkapa lililofanyika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip  Uwanja wa Ndege Zanzibar. 

Waziri wa Utalii Mhe.Simai  Mohammed Said akichangia mada ya  kuongezeka kwa kasi katika mikakati ya mabadiliko ya Sekta ya afya Tanzania kupitia Ushirika wa kibiashara na Sekta Binafsi wakati wa kongamano la kumbukizi ya maisha ya Rais wa Awamu ya tatu ambae pia ni muasisi na msarifu wa Tassisi ya Benjamin Mkapa Foundation (BMF) Hayati  Benjamin William Mkapa lililofanyika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip  Uwanja wa Ndege Zanzibar. 

Afisa Mtendaji Mkuu,Taasisi ya Mkapa (BMF)  dkt. Ellen Mkondya-Senkoro akizungumza wakati wa kongamano la kumbukizi ya maisha ya Rais wa Awamu ya tatu ambae pia ni muasisi na msarifu wa Tassisi ya Benjamin Mkapa Foundation (BMF) Hayati  Benjamin William Mkapa lililofanyika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip  Uwanja wa Ndege Zanzibar. 

Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu  akizungumza wakati wa kongamano la kumbukizi ya maisha ya Rais wa Awamu ya tatu ambae pia ni muasisi na msarifu wa Tassisi ya Benjamin Mkapa Foundation (BMF) Hayati  Benjamin William Mkapa lililofanyika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip  Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Daktari maalum wa Mifupa Hospitali ya Muhimbili Shadrak. S.Mwaibambe akichangia mada ya  kuongezeka kwa kasi katika mikakati ya mabadiliko ya Sekta ya afya Tanzania kupitia Ushirika wa kibiashara na Sekta Binafsi wakati wa kongamano la kumbukizi ya maisha ya Rais wa Awamu ya tatu ambae pia ni muasisi na msarifu wa Tassisi ya Benjamin Mkapa Foundation (BMF) Hayati  Benjamin William Mkapa lililofanyika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip  Uwanja wa Ndege Zanzibar.

***********************

NA ALI ISSA MAELEZO ZANZIBAR    

Makamu wa kwanza wa Rais Othman Masoud Othman, amesema hayati Benjameni William Mkapa hatoweza kusahaulika kwa sababu ni mtu aliyeibadilisha Tanzania katika nyanja nyingi kupitia uongozi wake uliofanya mageuzi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Masoud aliyasema hayo wakati akifungua kongamano la kumbukizi ya maisha ya  Rais wa awamu ya  tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Benjameni Mkapa katika hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege.

Alisema hayati Benjameni Mkapa alifuata mipango ya kufufua uchumi, sera thabiti za uchumi mkuu pamoja na mageuzi ya kimuundo wa  sera ya ubinafsishaji iliyoanzishwa na mtangulizi wake.

Alifahamisha kuwa  utawala wake ulipata misingi ya uchumi mkuu ambayo iliongeza imani ya wawekezaji kwa Nchi na Serikali, hivyo kutokana na juhudi hizo wamekusanyika kutafakari na kuweka mikakati juu ya nafasi ya sekta binafsi katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia uwekezaji katika sekta ya Afya.

Aidha alisema hayati Mkapa alitoa mchango mkubwa katika kuimarisha tasisi za uwajibikaji na kubadilisha sekta ya umma ambayo ilichochea ukuaji wa sekta binafsi.

Alisema siku hizo mbili zimewakutanisha pamoja na kutafakari juhudi za kuboresha utendaji kazi wa sekta ya afya jambo ambalo ni mwanga wa matumaini kwa watanzania wote hasa wale wanaoishi maeneo ya pembezoni na maeneo yasio na huduma.

Alifahamisha kwamba anaamini kumbukizi zitatumika kuheshimu maisha yake na kuyaenzi maono yake ya kuboresha hali ya kiuchumi na kijamii ili kupata mamilioni ya huduma Bora za afya kwa wanawake na wanaumme.

“Nimeambiwa kuwa kupitia jukwaa hili washiriki watajadili na kuchangia maoni ya kisera na kimakakati juu ya kujenga sera na mifumo thabit ya maendeleo ya uchumi wa Jamii huku mkiimarisha ulinzi wa kijamii kwa afya kupitia ushirikiano wa kimakakati kati ya serikali zetu kitaifa na kimataifa,” alisema.

Makamu Othman alisema SMT na SMZ zinatambua kuwa ushiriki mkubwa wa sekta na wadau wasiokuwa wa kisherikali kupitia Muungano wa biashara na PPPs katika kutoa huduma Bora za uhakika na nafuu ni misingi kwa  ukuaji mpana wa huduma na afya endelevu.

Alisema licha ya mafanikio kadhaa makubwa katika sekta ya uchumi na kijamii nchi katika kufafanua maono yake juu ya Muungano wa sekta binafsi PPPs kwa kukaribisha uwekezaji wa kimkakati zaidi kutoka sekta ya Fedha ili kuwekeza katika afya na kusaidia katika maeneo mengine ya kipaumbele kwa sekta mbalimbali hasa huduma za afya.

Hivyo aliahidi kwamba serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi yanayofaa kuongeza sekta za umma na binafsi na kuwekeza kwenye masulihisho ya kibunifu yanayoweza kutekelezeka ambayo yatabadilisha mfumo wa huduma za afya hasa kwa wanawake na watoto.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tasisi ya Benjameni Mkapa Dk. Ellen Mkondya alisema ni miaka miwili bila ya kuwa na Mkapa ni mambo mengi ambayo yanakumbukwa wakati wa uhai wake.

Alisema Rais Mkapa ndie muasisi uwekezaji wa sekta binafsi (PPP) ambapo wakati wake ndipo alipokaribisha wawekezaji katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wa afya alisema tasisi hiyo ilianzishwa kwa ajili ya kuboresha huduma za afya hususan upande wa ugonjwa wa ukimwi lakini muda unavyokwenda tasisi hiyo imepanua huduma zake ikiwemo utoaji wa mafunzo na kuboresha miundombinu ya afya.

Mapema Waziri wa Afya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Ummi Mwalimu, alisema wanatambua mchango mkubwa unaotolewa na tasisi binafsi katika sekta ya afya hivyo kongamano hilo liwe ni chachu katika kuongeza juhudi ya kusaidia jamii.

Alisema kupitia tasisi hiyo ambayo imeasisiwa na Rais Mkapa yapo maendeleo mengi yaliyofikiwa sio tu sekta ya afya pekee bali pia kwenye kukuza uchumi wa taifa.

Alisema wakati wa uhai wake zipo huduma nyingi ambazo zimeboreshwa katika miundombinu ya afya na huduma mbalimbali za Jamii kwa ujumla.

Naye Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed  Mazrui, alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweza kunufaika kupitia tasisi ya Mkapa imesaidia kuboresha huduma za Afya na  kuweza kuajiri manasi 37 kwa ajili ya kuhudumia jamii hasa katika maeneo ya vijini kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi Unguja na Pemba.

Alisema serikali itaendelea kutoa huduma bora kuanzia hospitali za wilaya na rufaa kwa kuweka vifaa tiba dawa na kutoa mafunzo kwa watendaji wake.

Waziri Mazrui alisema serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia kwa Rais Mwinyi inaweka mkazo katika kuhakikisha huduma za afya zinaboteka kwa wananchi jambo ambalo litasaidia kuleta maendeleo ya haraka kwa wazanzibari.

Alisema katika kuboresha huduma hizo serikali inajenga hospitali za wilaya 11 kwa Unguja na Pemba ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na za kiwango cha juu.

Alishukuru serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuwapatia mgao wa Fedha za uviko 19 ambazo zimesaidia katika kuboresha miundombinu ya afya nchini ambapo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu huduma za afya zitaboreka kuanzia ngazi ya msingi hadi rufaa ikiwemo upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

About the author

mzalendoeditor