Featured Kitaifa

MAAFISA TAKWIMU WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,akizungumza wakati akifunga kikao kazi cha Maafisa wanaoshughulikia masuala ya Takwimu na Mifumo ya kielektroniki (Maji App) katika sekta ya maji kilichomalizika leo Julai 13,2022 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati akifunga kikao kazi cha Maafisa wanaoshughulikia masuala ya Takwimu na Mifumo ya kielektroniki (Maji App) katika sekta ya maji kilichomalizika leo Julai 13,2022 jijini Dodoma.

MKURUGENZI wa Mipango kutoka Wizara ya Maji Bw.Prosper Buchafwe,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Maafisa wanaoshughulikia masuala ya Takwimu na Mifumo ya kielektroniki (Maji App) katika sekta ya maji kilichomalizika leo Julai 13,2022 jijini Dodoma.

Mhaidrolojia Mkuu Bodi ya Maji Bonde la Pangani,Philipo Patrick,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Maafisa wanaoshughulikia masuala ya Takwimu na Mifumo ya kielektroniki (Maji App) katika sekta ya maji kilichomalizika leo Julai 13,2022 jijini Dodoma.

MKUU wa TEHAMA kutoka Wizara ya Maji Joash Nyitambe ,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Maafisa wanaoshughulikia masuala ya Takwimu na Mifumo ya kielektroniki (Maji App) katika sekta ya maji kilichomalizika leo Julai 13,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri  wa Maji Jumaa Aweso (hayupo pichani) wakati akifunga kikao kazi cha Maafisa wanaoshughulikia masuala ya Takwimu na Mifumo ya kielektroniki (Maji App) katika sekta ya maji kilichomalizika leo Julai 13,2022 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga kikao kazi cha Maafisa wanaoshughulikia masuala ya Takwimu na Mifumo ya kielektroniki (Maji App) katika sekta ya maji kilichomalizika leo Julai 13,2022 jijini Dodoma.

………………………………………

Na Odilo Bolgas-DODOMA

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ,amewataka Maafisa Takwimu kufanya kazi kwa ufanisi,weledi pamoja na kujituma ili umuhimu wao uonekane katika wizara hiyo.

Kauli hiyo ameitoa leo Julai 7,2022 wakati akifunga kikao kazi cha Maafisa wanaoshughulikia masuala ya Takwimu na Mifumo ya kielektroniki (Maji App) katika sekta ya maji kilichofanyika jijini Dodoma.

Waziri  Aweso amewataka kufanya kazi kwa ushirikiano kwa Wizara ya Maji ili waweze kuonekana zaidi.

“Lazima muone kwamba hii kazi nimepewa lakini wapo wengi wanaoweza kufanya kazi hii,hivyo kafanyeni kazi yenye tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.”aamesema Aweso

Aidha  amewaagiza maafisa mifumo ya kielektroniki kutengeneza mifumo ya kuwatambua watu wanaohusika kufanya hivyo lakini hawafanyi kwa makusudi.

“Wapo watu wanaotakiwa ku-update takwimu lakini hawafanyi hivyo kwa makusudi,utengenezwe mfumo wa kutambua kwamba hawafanyi hivyo,lakini pia kuwatambua ambao wanaweka takwimu ambazo siyo sahihi”ameeleza Aweso

Hata hivyo Waziri Aweso amewaagiza viongoziwa wizara hiyo kuhakikisha wanaweka mazingira wezeshi kwa maafisa takwimu ili waweze kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi.

“Bila takwimu watu watakuwa wanapika data tu ..,hata gari ili liende linahitaji mafuta hata kama ni lita moja,sasa watu hawa wawezeshwe ili kufanikisha majukumu yao.”amesema  Aweso

“Watu wa takwimu katika wizara yetu ni muhimu na hawapo hapa kwa bahati mbaya ,ni muhimu na mahsusi katika kufanikisha utatuzi wa changamoto zilizopo katika wizarani.”

Hata hivyo Aweso amewataka watumishi wote katika taasisi zake kupenda na kushirikiana katika utendaji kazi wao.

About the author

mzalendoeditor