Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AHUTUBIA MAADHIMISHO YA MKUTANO WA 20 WA SHIRIKISHO LA MABARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI AFRIKA MASHARIKI NA KATI (AMECEA) JIJINI DAR ES SALAAM

Written by mzalendoeditor

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Maaskofu kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika pamoja na baadhi ya viongozi katika maadhimisho ya mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) uliofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsalimia Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Muadhama Kardinali Polycarp Pengo kwenye maadhimisho ya mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) uliofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre Jijini Dar es Salaam

Maaskofu wa Kanisa Katoliki kutoka nchi mbalimbali pamoja na Wageni wengine wakiwa kwenye maadhimisho ya mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) uliofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre Jijini Dar es Salaam.

……………………………………..

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewataka Viongozi wa dini na kisiasa pamoja na waumini kuhakikisha wanadumisha amani na kutunza mazingira nchini. 

Rais Samia ametoa wito huo leo wakati wa maadhimisho ya mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) akisisitiza kuwa uwepo wa amani nchini unasaidia kutunza ikolojia.

Aidha, Rais Samia amesema uharibifu wa mazingiza kama ukataji miti huathiri hali ya hewa duniani ikiwemo kina cha bahari hivyo ni wajibu wetu kulinda mazingira ili kutohatarisha maendeleo yetu. 

Rais Samia pia amesema hatuna budi kutunza vyanzo vya maji na misitu, kupanda miti na kuhakikisha mazingira ya maeneo yanayotuzunguka yanasafishwa katika miji yote kama inavyoelekezwa kwenye Sera ya Taifa ya Mazingira.  

Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema Serikali ya Tanzania inafuata siasa ya maendeleo jumuishi (inclusive development policy), hivyo ipo tayari kuzipokea na kufanya kazi na taasisi zisizo za kiserikali zikiwemo za kidini na kijamii ili kufikia mustakabali mwema wa maisha na maendeleo ya mwanadamu.

Rais Samia ametoa wito kwa Viongozi wa kidini kuendelea kutekeleza kwa vitendo Malengo Endelevu 17 ya Dunia na Malengo ya Umoja wa Afrika (AU) ikiwemo utunzaji wa mazingira.

About the author

mzalendoeditor